Kuwa Makini na Unaowaona Kama Role Model

Shalom
Leo nimewiwa kusema na vijana. Vijana wengi hutafuta mtu aliyefanikiwa ili aweze kuwa motisha na kuwatia moyo kufanikiwa, hili ni jambo zuri maana hata elisha alifuatana na eliya akitafuta kufanikiwa kama yeye na hata aliomba apewe nguvu maradufu ya iliyokuwa kwa eliya. Eliya alikuwa role model wake. Tatizo linakuja vijana wengi wanatafuta role model kwa kuangalia hali ya sasa ya muhusika (final product) na sio safari ya muhusika kufika hapo alipo( journey).

Unapoangalia hali ya sasa na kuona mtu aliyefanikiwa na kusahau kuangalia safari yake unaweza kujikuta una role model ambaye kiuhakika hafai kukuhamasisha kabisa. Dunia ya sasa inawasherehekea watu wenye pesa, vyeo na madaraka bila kujali vimepatikana vipi. Watu hawaangalii safari bali mwisho wa safari. Hali hii imepelekea vijana kuwa na role model ambao kiuhakika ukiangalia maisha yao hakuna hata kimoja kinachopaswa kuigwa, watu wamefika walipo kwa njia nyingi sana za mkato ambazo hazimpendezi Mungu.

Tafuta sana kujua aliyefanikiwa kafanikiwaje na usiingie kwenye mkumbo wa kumsifia mtu kisa unamuona anahela na anatumia media kusaidia watu bila kujua amefikaje hapo alipofika. Tunapaswa kujifunza kwa wale waliotutangulia kwa kuangalia mwenendo wao na kujifunza jinsi wanavyofanya kazi kwa bidii, wanavyotumia fursa vizuri na wanavyoukomboa wakati lakini yote yawe katika kumpendeza Mungu. Wapo wengi sana wanaofaa kuwa role models kwa vijana lakini sababu media hazijawabeba basi vijana wanaona kama hawafai. Angalia waliokuzunguka na utaona wengi sana unaoweza kujifunza kutoka kwao.

Advertisements

One thought on “Kuwa Makini na Unaowaona Kama Role Model

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s