Sifa Njema za Msichana / Mwanamke

Ibrahimu alimuagiza mtumishi wake amtafutue mtoto wake isaka mke kutoka katika watu wa Israel. Alipoenda yule mtumishi aliomba Mungu ampatie mwanamke ambaye atakuwa tayari kumpa maji yeye na ngamia wake. Ni kwanini mtu huyu aliomba mwanamke wa aina hii? Mwanamke huyu lazima atakuwa na sifa zifuatazo:

1. Mwenye upendo na anayejali mahitaji ya watu wengine.
Sio rahisi mtu asiye na upendo na asiyejali mahitaji ya watu kumsikiliza mgeni ma kumpa maji yeye na ngamia zake. Mwingine angesema chota mwenyewe mimi nina haraka zangu. Bint unapotaka Mungu akupe mchumba yapasa uwe mwenye upendo na kujali mahitaji ya watu bila kuangalia unapata nini.

2. Mchapakazi
Ngamia mmoja anakunywa maji mengi sana sasa kuwanywesha ngamia kumi sio kazi ndogo. Bint huyu alikuwa mchapakazi ndio maana hakuona shida. Wasichana wengi siku hizi ni wavivu na hawapendi kazi, kama unafikiria kuolewa na kuwa na familia yako uchapakazi hauwezi kuepukika na waoaji Mara nyingi hutafuta binti mchapakazi. Utawezaje kumhudumia mume, watoto, wakwe na mambo yote yanayokuhusu kama wewe ni mvivu?? Badilika!

3. Mkarimu
Baada ya hayo yote aliwakaribisha nyumbani kwa ajili ya kupumzika na pia aliwahahakishia malisho ya ngamia. Hakuishia hapo alitoa taarifa nyumbani na kuwaandalia wageni mapokezi mazuri. Utakapoolewa tegemea wageni mbalimbali, bila ukarimu hutaweza kukaa na watu na hutaweza kujenga mahusiano mazuri.

Kila binti na kila mwanamke ahakikishe anasifa hizi tatu, ni muhimu sana ili kuwa na familia yenye mafanikio.

MWA. 24:15, 17-20, 25
“Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Ibrahimu, naye ana mtungi begani pake. Ndipo yule mtumishi akapiga mbio kwenda kumlaki, akasema, Tafadhali unipe maji kidogo katika mtungi wako ninywe. Naye akasema, Unywe, bwana wangu, akafanya haraka, akatua mtungi wake mkononi mwake, akamnywesha. Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia zako nitawatekea, hata watakapokwisha kunywa. Akafanya haraka, akamwaga maji ya mtungi wake katika birika, akapiga mbio kisimani ateke, akawatekea ngamia zake wote. Tena akamwambia, Kwetu kuna majani na malisho ya kutosha, na mahali pa kukaa wageni.”

One thought on “Sifa Njema za Msichana / Mwanamke

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s