Ishi Kwa Heshima na Watu Wanaokulea

Katika somo lililopita niliongelea ukarimu, kuwa kila mwanamke anapaswa kuwa mkarimu kwa watu wa nyumbani kwake na wote wanaomzunguka. Sasa leo niongelee upande wa pili. Wengi wetu tumewahi kuishi nyumbani kwa ndugu na jamaa na wengine bado tunaoshi kwao maana kwa jamii yetu jambo hili halikwepeki.

Ni vyema unapoishi na mtu kitu cha kwanza uisome familia hiyo na hasa mama mwenye nyumba nini hapendi na nini kinamkasirisha. Huwezi kuishi na amani kwa mtu kama utaenda kinyume na mama wa hapo nyumbani. Lazima uhakikishe unaishi kwa amani naye na kikubwa ni kumheshimu kama mzazi wako. Anaishi na wewe na kuangalia unakula, unalala upo salama inatosha, usitake makuu kama vile upo kwako na kuanza kiburi sababu ya hili na lile. Mshukuru Mungu kwa hilo na kama unapata ya ziada tambua ni kwa neema tu na kumshukuru Mungu.

Kuna watu wanatabia ya kumzarau mama kama ndugu yao wa damu ni baba mwenye hiyo nyumba. Kumbuka unavyowatendea wengine nawe utakuja kutendewa. Onyesha moyo wa shukrani, uwe na bidii ya kazi na msikivu. Hakuna mtu atakayeona shida kukaa na mtu msikivu, mchapakazi na mtii. Wengi wanalalamika fulani ananitesa, fulani hanipendi lakini ukichunguza utaona wao ndio chanzo. Usijenge kiburi kwa ndugu yako maana kamwe huwezi kujenga kiburi kwa mzazi wako, mchukulie kama mzazi wako na utaona baraka za Mungu juu yako.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s