Usilazimishe Sherehe Kuzidi Uwezo Wako

Ushauri kwa wasichana:
Nimeona watu wengi wakihangaika kutumia kila hela waliyonayo hadi wakati mwingine kuingia kwenye madeni ili tu wawe na kitchen party kama ya fulani, send off ya mwaka na harusi ya karne. Wasichana wamewaingiza wachumba wao madeni yasiyo ya lazima kwa ajili tu ya sherehe za harusi. Wanasahau kuwa ndoa wanayoianza itahitaji akiba ya kutosha na maisha hayaishii kwenye ukumbi wa sherehe bali ndio kwanza yanaanza.

Kuna haja gani ya kufanya sherehe tatu nne kama uwezo wa kufanya hivyo haupo matokeo yake unaishia kuwaona watu wabaya?? Kwanini utake kuvaa nguo na viatu vya mamilioni ya fedha wakati uwezo wenu hauruhusu hadi inafikia mtu anakopa hela ili anunue nguo au mapambo ya harusi??? Wakati wa maandalizi ya harusi ni wakati wa kuhakikisha unasave hela uwezavyo, achana na manunuzi yasiyo ya lazima na kufuata mkumbo. Hata ukifanya harusi ya Gharama kiasi gani baada ya muda mawimbi yake yataisha na yataonekana ya mwingine ambaye anakuja nyuma yako.

Fanya harusi kulingana na uwezo wako, iwe ya kifahari sana, kawaida au ndogo kabisa ikilingana na uwezo hako haitakupa stress wala kukuingiza kwenye madeni ambayo yatachukua muda kuyalipa na yatakuchelewesha kufanya mambo ya maendeleo kwenye maisha yako mapya. Usilazimishe jambo ambalo litakugharimu furaha, amani na mahusiano mazuri na watu. 

One thought on “Usilazimishe Sherehe Kuzidi Uwezo Wako

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s