Kijana Tunza Wokovu Wako

Nataka niongee na vijana anaosema wameokoka, wa kike kwa wa kiume. Unakiri umeokoka, unatumika nyumbani mwa Bwana kanisani na kwenye huduma mbalimbali. Unaongoza sifa, unaimba sifa, anapiga vyombo, unahubiri, shemasi na mengine mwengi na unategemewa hasa katika mwili wa Kristo. Ila sasa pale unapopata mchumba au unapoona kuwa umepata mchumba unasahau kabisa kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu, umezibeba chapa ya Yesu, chumvi ya ulimwengu.

Yani vijana wa siku hizi wakishaambiana nakupenda nitakuoa wanaona tayari wameshaoana. Ile tabia ya watoto wa Mungu inapotea kabisa ndani yao, wanaanza kuishi sawa na watu wasiomjua Mungu. Bado hamjafunga ndoa ila kila siku upo nyumbani kwa kaka huyo anapika, unafua na kufanya usafi, hamjaoana ila mkiwa peke yenu mnashikana shikana, kupigana mabusu na kuamshana hisia kabla ya wakati wake.

Kila saa mnachat habari za sex, na mambo yanayofanana na hayo, hadi kutumiana picha zisizofaa. Upo wapi wokovu wako? Kwanini umkosee Mungu kwa jambo ambalo unaweza kusubiri wakati wake ufike? Hivi baada ya kuchat hivyo mnavyochat baada ya kutenda hayo mnayotenda, unapata ujasiri wa kusimama mbele za Mungu??

Mungu awasaidie sana vijana wa kizazi cha sasa.

Advertisements

2 thoughts on “Kijana Tunza Wokovu Wako

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s