Matarajio ya Ndoa

Mtu anapokuwa kwenye mandalizi ya kuingia kwenye ndoa anakuwa na matarajio mengi sana. Yani anaona kama anachelewa kuingia kwenye ndoa akapate yale anayoyatarajia na kuyatazamia. Hakuna mtu anaingia kwenye ndoa akiwa na mawazo kwamba mwezangu atakuwa na hili na lile ambayo yatafanya matarajio yake yasiwe kama anavyofikiri. Mwanaume anatarajia na kuwaza kuwa nitakuwa na mke anayenipikia chakula kitamu, anayepanga nyumba vizuri na msafi, anayejali ndugu zangu na kuwakaribisha kwa upendo na wadogo zangu watapata mtu wa kuwalea pamoja nami, yatafanya hiki na kile n.k. Msichana naye anatarajia atapata mtu atakaye mtunza na kumlinda, mtu atakayekuwa kiongozi wa familia, mtu watakaye saidiana kazi za nyumbani, watapika pamoja na kucheka, mtu atakaye mfanya ajione kama malkia, mtu atakaye msikiliza n.k.

Sasa kasheshe inatokea pale wameshaoana mwanaume anagundua mkewe hana hobby ya kupika na sababu hawana watoto anapendelea kula restaurant, mke sio msafi kama alivyodhania, alikuwa anaishi na ndugu zake mke hataki anataka waishi peke yao, Mke naye anagundua kuwa mume sio mtoaji kirahisi hasa kwa mambo ya anasa, mume hapendi kabisa kusaidia kazi za nyumbani, mume anapovua nguo au sox anaacha hapo hapo alipokaa, mume ni msiri asiyependa kushauriwa,n.k. Hapo sasa kila mtu anaanza kulazimisha matarajio yake yafanikishwe, kila mmoja anasahau compromise na kuchukuliana bali ni kulaumiana na kuona kama hapendwi. Hata yale mambo ya ndoa ya faragha yanaanza kudhoofu maana mioyo imejaa matarajio yasiyofikika.

Kuna mambo ambayo yanatokana na malezi, makuzi na mitazamo na huwa hayaishi haraka mtu akiyazoea. Inabidi kuchukuliana kwa upendo, kutokuwa na expectations nyingi bali kujifunza kila mmoja kuhusu mwenzie na kuwa na positive mind mnapozungumzia tofauti zenu. Usilazimishe ndoa yako iwe kama ya fulani, fahamu nini kinafaa kwako, nini kitaboresha kwako na uwe flexible kujifunza, kupokea mambo mapya na kutoa zaidi ya kupokea. Trust me ndoa inaanza kwenye maisha mnayoishi kila siku, mnavyoshirikishana, saidiana, kujaliana na kuchukuliana, na sio kny faragha. Haya ndiyo yanaboresha faragha au kuiua kabisa.

Advertisements

One thought on “Matarajio ya Ndoa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s