Mke Anaposahaulika – Mke wa Nuhu

Biblia imeelezea kwa kirefu habari ya nuhu na safina. Jinsi nuhu alivyomcha Mungu, alivyoijenga safina na kuokolewa na gharika kuu yeye na familia yake. Lakini haielezei kwa kina habari za mke wa nuhu, wala haituambii jina lake. Katika hali ya kawaida ni lazima mke wa nuhu alivumilia kuona mume wake akichekwa na watu wakati anajenga safina, jambo hili lazima lilimuumiza kuona watu wanamdhihaki mume wake. Alikuwa pamoja na mume wake katika hali zote hadi kuishi na wanyama kwenye safina. Na baada ya gharika kuisha, alikuwa pamoja na mumewe kuanza maisha upya baada ya kila kitu kukumbwa na mafuriko. Haikuwa rahisi hata kidogo.

Wake za watumishi wataelewa zaidi jinsi gani unajisikia pale ambapo unamsapoti mumeo kwa kila hali ila watu hawaoni umuhimu wako na pengine hawajui hata jina lako. Wanawake wengi wamekuwa sababu ya mafanikio ya waume zao kwa kuwaamini, kuwapa nafasi, kuwashauri na kuwaombea lakini hakuna anayetambua mchango wao na wanabaki kuwa invisible. Usikate tamaa wala kuvunjika moyo, Mungu anaiona na kuitambua kazi yako na mchango wako katika mafanikio ya mumeo na familia. Japokuwa wanadamu watausahau mchango wako Mungu hatasahau kamwe.

Mume ni vizuri ukatambua na kukiri mchango wa mke wako katika maisha yako, kufanya hivyo kutainua nafsi yake na kumfanya azidi kukusapoti zaidi na zaidi.

Advertisements

2 thoughts on “Mke Anaposahaulika – Mke wa Nuhu

 1. Nakubaliana sana na hili,Je ni sawa wake za watumishi kuitwa “Mama Mchungaji ….”au aitwe Jina lake ?mfano Lucy na jina la mumewe? Naona kuitwa mama Mchungaji/mtumishi linachangia hata jina lake kutojulikana kwa watu.”Utambulisho wako ni jina lako”

  Angelina Stephen
  Compassion International Tanzania
  Partnership Training and support Manager
  P.O.Box 3064
  Arusha
  Email:astephen@tz.ci.org
  Email:myangelika2000@yahoo.com
  Skype:angelstephen11

 2. kusimama katika kweli ya Mungu kunaleta faraja, hata kama wanadamu wanakuona hufai.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s