Yesu Anarudi Mpendwa…

Tafuta sana kuwa karibu na Mungu. Tafuta sana kujaa nguvu za Roho mtakatifu wakati wote. Tafuta sana kujawa na neno la Mungu siku zote. Ukijawa na maneno ya Mungu, nguvu za Roho mtakatifu na kuwa karibu na Mungu hautahitaji mchungaji kukuambia kuwa jambo fulani ni dhambi. Hautahitaji mke/mume akuambie jambo fulani sio sawa, hautahitaji kiongozi wa kanisa akuambie kuwa unavyochat unakosea wala hautahitaji mshirika akuone ndio ukiri kuwa umefanya dhambi.

Roho mtakatifu hutushuhudia ndani kwa habari ya dhambi, yani pale unapowaza tu Roho mtakatifu anakushuhudia kuwa si sawa na kwa sababu unamfuata pale pale unaacha na kutubu. Walokole wa leo wamezoelea dhambi, yani hata ukimkamata atakuuliza wapi ushahidi, wanandoa wanaona kucheat sio tatizo ila pale mwenzi wake aligundua ndio wanaumia na kujuta.

Upo wapi wokovu wa kwanza? Je injili ya mafanikio imetupumbaza hadi tukasahau kwanini tumeokoka na hasa nini msingi wa safari yetu? Je Yesu akirudi sasa hivi jiulize utaenda naye au utabaki? Yesu anarudi mara ya pili kulichukua kanisa, hii ni kweli na hakika. Je ni nini hasa kinakuzuia usimuone Mungu? Yatafakari maisha yako na uchukue hatua ya busara kungali mapema.

5 thoughts on “Yesu Anarudi Mpendwa…

  1. shalom wapendwa,napenda tushahuliane kwa wale walio mjuwa mungu kama WACHUNGAJI,PASTORS,WAOMBAJI,WANABII,hawa watu wanajuwa neon la mungu kabisa bila kukwepa ao kujitetea,wao ndo wakuwalisha wakristo katika kiroho,lakini chakushangaa hawa watumishi wanahubiri kuhusu mazuri hawahubiri kuhusu mabaya.wanaficha mabaya yanayo mchukiza mungu halafu wanafurahia yanayo mchukiza mungu.jamani wachungaji na manabii na mapastors wanajuwa kwamba mwanamke kuvaa suruwali ni chukizo kwa mungu kuva nguo yoyote isiyo ya heshima ni dhambi,wanajuwa kwamba majipambo ya mwili na kubadilisha ngozi ya mwili ni chukizo kwa mungu wanafahamu vizuri maana wanajuwa biblia inasema nini na isitoshe wanaongea na mungu lakini hawahubiri kwamba hayo yote ni chukizo kwa mungu.usipoambia watu ukweli kutoka ndani ya ya biblia damu yawo iko ku vichwa yenu maana munaficha mapenzi ya mungu ndani yenu hamsemi kinacho mchukiza mungu.mwanamke yeyote anatakiwa kumpendeza mungu akiwa amefunika kichwa yake na kuvaa nguo za heshima maana mwili ni hekalu la mungu takatifu. kuvaa suruwali kwa mwanamke haimpendezi mungu,tubadilisha nywele,kujicream,kichwa wazi,mavipodozi,mahereni,pete ,shedo ,kusuka nywele na vinginevyo ni chukizo kwa mungu na kama unafanya hivyo mbingu siyo yako mama ao dada.na kama wachungaji hawaubiri kuhusu hivyo kwamba si vibaya hawatamuona mungu na damu ya wengi iko juu yao watasamba na mungu kwasababu hawakuwambia watu ukweli. furahiya uzuri mungu aliyekupa maana ukitumia vipodozi na kusuka nywele na kuvaa pants hapo umemzalau aliye kuumba kwamba hakukuumba vizuri.fikiliya je mungu alikuumba ukiwa na make up kwenye mwili wako? je ulipo zaliwa nywele zako zilikuwa zimesukwa? ao ulikuwa na luster kwenye kichwa yako? lakini mungu alipendezwa na jisi alivyo kuumba,na wewe umedharau unajiwekea vipodozi ili uwe mrembo kuzidi ulivyo zaliwa.MUNGU ATUKUMBUKE SISI SOTE.

  2. ni kweli yesu yu karibu, tukeshe tukiomba ili akirudi atukute tayari kwenda nae.

  3. Kweli Mungu atusaidie na tujae Roho Mtakatifu Mwalimu na kiongozi wa kweli,ktk nyakati hizi za hatari

  4. Muda huu si wa kutegemea wachungaji angalia neon la Mungu na ulinsimamie kwa ujasiri wote

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s