Scars / Makovu

Scars / Makovu
Kovu ni ushahidi kuwa palikua na kidonda. Kila kidonda huacha kovu ila makovu hutofautiana ukubwa kulingana na ukubwa wa kidonda. Makovu mengine hupotea baada ya siku kadhaa, mengine week, miezi, mengine huchukua miaka kupotea na kuna mengine hayapotei kabisa
yananabaki siku zote. Kawaida kovu halina maumivu, kama kuna maumivu basi bado ni kidonda na hakijapona, kovu huwa kama kumbukumbu tu lakini isiyo na maumivu.

Kuna sababu nyingi zinazoleta vidonda vinavyoacha makovu. Kuna makovu yanayoachwa na vidonda vilivyopatikana katika kujifunza, kujifunza vitu ambayo ni lazima uvipitie mfano mtoto anayejifunza kutembea anaponguka na kuumia, unapojifunza kuendesha baiskeli n.k. bila kujifunza huwezi kufahamu na katika kujifunza unakutana na vidonda vinavyoacha makovu. Makovu mengine yanapatikana katika kufanya yale unayopaswa kufanya/ katika kazi unazofanya mfano kupika ukaungua, unajenga nyumba ukaumia n.k. na kuna makovu yanapatikana kutokana na kusababishwa na watu wengine, kusukumwa ukaumia, kupigwa n.k na mwisho makovu yatokanayo na vidonda ulivyopata wakati unamsaidia mtu.

Vidonda vya makovu haya yote vinauma, lakini kuna ambavyo maumivu yanaishia mwilini na mengine yanaingia hadi rohoni. Katika maisha yetu ya kawaida pia tunakutana na kuumia kwingi, kunaacha makovu ya aina mbalimbali. Makovu mengine unayasahau baada ya muda mfupi lakini mengine hayaondoki kabisa. Unaweza kuumizwa unapotafuta kazi ukatendewa jambo ambalo likakuumiza sana lakini baada ya kupata kazi ukasahau kabisa, au ukaumia katika masomo yako, hali ikawa mbaya lakini unapokuja kumaliza na kufaulu unasahau yote. Ila kuna maumivu hasa ya kutendwa na mchumba, kutengwa na ndugu, kuachwa baada ya kuvalishwa pete, kutendwa na mume au mke, kufukuzwa kazi bila kosa, n.k ambayo Mara nyingi hukaa muda mrefu au kutokuisha kabisa.

Katika haya yote unapaswa kuzingatia kuwa kovu halina maumivu. Litakuwepo pale kukukumbusha kuwa ulipitia haya na sasa umevuka, kukuonya kuwa usipite mahali fulani utaumia na kukutia moyo kuwa yamepita na sasa ni mshindi. Kumbuka kovu halina maumivu. Kovu ni kumbukumbu na sio kizigiti. Kuna watu wameacha makovu yawe vizingiti vya kuwazuia kusonga mbele. Kama kovu lina maumivu tambua kidonda hakijapona. Muende Bwana Yesu tabibu wa kweli akuponye kidonda na kuondoa maumivu yote. Kidonda kilichopona kovu haliumi. Kovu halionyeshi kesho yako itakuwaje bali linaonyesha jana umepitia nini. Usifungwe na kovu bali likufanye uzidi kusonga mbele.

Advertisements

2 thoughts on “Scars / Makovu

  1. bwana yesu ndio jibu la matatizo yetu,alijitwika dhambi zetu pale msalabani ili wanadamu tukombelewe hivyo hatuna budi kumkimbilia wakati wote

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s