Hausikilizwi?? Mueleze Mungu Aingilie Kati

Unapoona kuwa mwenzi wako hakubaliani na wazo lako na hasa hii huwatokea wake zaidi, pale unampa mume wako ushauri bora kwa manufaa ya familia yeye anaona kuwa sio sawa na hakubaliani nawe, muendee Mungu na kumueleza jambo hilo. Muombe Mungu aingilie kati kama alivyofanya kwa Sara pale ibrahim alipokuwa hakubaliani na wazo lake la kumuondoa Ishmael.

Sarah alipoona hali sio nzuri kati ya Ishmael na isaka akamueleza Ibrahim amfukuze hajiri na mwanaye. Ibrahim hakukubali hadi pale Mungu alipozungumza naye. Biblia inasema neno lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahim, inawezekana kabisa palitokea malumbano na mabishano kati yao hadi Mungu alipoingilia kati. Pale unapoona mumeo hakuungi mkono wala kukubali ushauri wako, mueleze Mungu naye ataingilia kati. Nimependa sana pale Mungu alipomwambia ibrahim, “kila akuambialo Sara sikiliza sauti yake”..

MWA. 21:9-12
“Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka. Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka. Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.”

Advertisements

One thought on “Hausikilizwi?? Mueleze Mungu Aingilie Kati

  1. Pia kama mume hakubalianai na ushauri wako wamama tusiwe ving’ang’nizi , wakali na kufanya kwa lazima akikataa leo mwendee kesho kwa unyenyekevu zaidi na upole wakati huo ukumbuke kusugua goti kwa aliyemuumba asiyeshindwa kitu chochote. Hata kama unapesa yako mkubaliane na hilo jambo litakuwa na Baraka Pia huenda Mungu anakuepushia kitu Fulani usifanye kitu kwa akili yako ya kibinadamu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s