Mungu Ni Kimbilio Na Nguvu

Napenda nikutie moyo wewe mzazi ambaye unauguza mtoto na hasa wale ambao watoto wao wana magonjwa ya kuwafanya wateseke kwa muda mrefu. Hakuna kitu kigumu kama kumuona mtoto wako anateseka nawe huna cha kufanya. Kuna watoto wanateseka na kansa, vidonda vya kuungua, ajali, na magonjwa mengine mbalimbali. Wazazi hawa wanahitaji maombi yetu sana sana, kibinadamu wanaumia sana na kuchoka sana.

Mungu awatie nguvu, Mungu awakumbuke, Mungu awaponye watoto wenu na pia Mungu awape nguvu na neema ya kukabiliana na jambo hilo. Mungu yupo upande wako usikate tamaa, endelea kusimama katika nafasi yako kama mzazi bila kukata tamaa, sisi tunakuombea. Ni njema na inapendeza ukiweza kumtembelea mzazi wa aina hii, mfariji na pia msaidie gharama za matibabu kadiri unavyoweza, hakika wanahitaji sana faraja na maombi na msaada pale inapobidi.

ZAB. 46:1-2, 11
“Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.  Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.  BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.”

EZR. 10:4
“Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s