Muombee Anayepita Katika Magumu

Binadamu tumeumbwa na uwezo tofauti wa kukabili maumivu na magumu ya maisha. Kuna wengine wakipata magumu na maumivu ya moyo wanakuwa wakimya, wanayaweka moyoni na kulia ndani kwa ndani, wengine wanalia sanaaaa kisha maumivu yanaisha na wanaendelea na maisha, wengine wanajisahaulisha na kujifanya kama hawana tatizo (denial), wengine wanaongea sana na kumsimulia kila mtu, wengine wanaandika kwenye diary, wengine wanaharibu mali na kuvunja vunja vitu, wengine wanakula junk food…n.k.

Hatuwezi kumlaumu mtu kwa njia aliyoitumia kukabiliana na stress na maumivu maana wakati huo akili yake ya kawaida haifanyi kazi sawasawa, huu sio wakati wa kumwambia usifanye hivi fanya vile bali ni wakati wa kumpa usikivu na faraja isiyo na hukumu na kumuombea sana Mungu aifungue akili yake na moyo wake. Huu sio Wakati wa kumwambia mbona fulani lilimkuta kama hilo hakufanya hivyo, maana huyu sio fulani. Huu sio wakati wa kumgombeza au kumsimanga, ni wakati wa kumuonyesha unconditional love.

Biblia inasema tulie na wanaolia, muda wa kulia hahitaji kuambiwa wapi anakosea au nini amekosea bali mtu aliyetayari kulia pamoja naye na kisha kumnyanyua na kumuinua kwenye maombi.

Advertisements

One thought on “Muombee Anayepita Katika Magumu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s