Tafakari ya Ndoa

Hili jambo huniwazisha sana. Ni kawaida kabisa pale ambapo mwanaume anapotoka nje ya ndoa basi watu wote wanawake kwa wanaume watamlaumu mke wake kuwa ni chanzo. Hali hii imezoeleka hadi kupelekea wanawake kukaa kimya na kutosema hata kwa wachungaji wao pale waume zao wanapotoka nje ya ndoa hata kama kwa kurudi rudia kuogopa kualaumiwa. Pia hali hii imewafanya wanawake wengi kuishi kwa woga kwenye ndoa zao maana jamii na wanaume wamehalalisha kuwa kama mke hamfurahishi mumewe katika kila nyanja basi mumewe atatoka nje. Mabinti wanafundishwa mumeo mfanyie hili na lile na usipofanya atatafuta nje. Yaani mkazo na msukumo hauwi ili wote mfurahie ndoa bali ili mwanaume asitoke nje.

Na mwanaume akitoka nje utasikia mke wangu hanifanyii hili na lile na kila mtu anakubali kweeeli hapo hukuwa na jinsi. Bado najiuliza kwa upande wa pili mbona hali ni tofauti? Sijawahi ona watu hakusema kuwa mwanamke anapotoka nje ni sababu ya mume wake, hata kama mumewe anamfanyia kila aina ya manyanyasho ataambiwa avumilie, najiuliza uvumilivu ni kwa wanawake tu au na wanaume Pia?

Ukiangalia kiapo cha ndoa kila mmoja anaapa kuwa mwaminifu kwa mwenzie katika hali zote, shida na raha, ila mwanaume katika shida tena ndogo sana anakimbilia kutafuta faraja nje ila mwanamke yeye anatakiwa kuvumilia. Najiuliza, hivi wanaume wao hawapaswi kushika kiapo cha ndoa?  Maana hali hii imewafanya Pia wanaume wengi kuwachukulia wake zao for granted yani mradi amemuoa basi kazi yake imeisha, hashughuliki kumfurahisha na kumfanya ajisikie wa thamani maana anajua hata asipofanya hivyo mkewe lazima atamfanyia mema kwa kuogopa mume atatoka nje. Wakati mwingine wanandoa wanapokosa mtoto mume atatafuta nje watu wanamulewa kuwa hakuwa na jinsi ila mke akifanya hivyo atapewa majina yote mabaya.

Tutafakari kwa pamoja, upo na mwenzi wako ili usitoke nje au upo naye sababu unampenda na utafanya kila uwezalo kumfurahisha?

Mwanaume utakuta anasema mke wangu mkorofi, mke wangu mkali, mke wangu hajui kupika, mke wangu hili na lile Ndio maana anatoka nje ila pale anapogundulika na mke anataka kuondoka anasema uliapa kukaa nami katika shida na raha, swali mbona wanaume hamkai na wake zenu katika shida???

YER. 9:17-18, 20-21
“BWANA wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje; na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji. Lakini lisikieni neno la BWANA, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia.  Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu.”

Advertisements

5 thoughts on “Tafakari ya Ndoa

  1. If your husband passed away and you are still young is it must to be married again?

  2. Hello, its a personal choice and not mandatory, I have witnessed some women chose to remain single

  3. Oooh!GOD have merce on us,because wthout us marriage is a taugh institution

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s