Mwanamke Usikate Tamaa Katika Majaribu

Wanawake kwenye ndoa wanapitia mitihani na majaribu mengi sana. Majaribu haya yapo katika kila hatua ya maisha na ni hakika ya kuwa mengine ni mazito sana na yanaumiza sana. Kuna majaribu ya kukosa mtoto, moyo unasononeka na ndugu wanakusimanga; Majaribu ya magonjwa kwa watoto, wengine watoto wanahitaji uangalizi maalumu hivyo huwaumiza sana; majaribu ya uzazi, kuanzia mimba hadi kujifungua nayo huumiza sana mwili.

Yako pia majaribu yanayoletwa na ndugu na jamaa, wakwe kwa wifi, yani wanaamua tu kutokukukubali, kukutafutia visa na kukuumiza. Mengine ni ya kipato, mambo yanayumba, ada za watoto zinakosekana, maisha yanakuwa magumu sana; bado hujakutana na ya wasichana wa kazi. Kubwa zaidi wengine jaribu lao kubwa ni mume, anaweza kuwa hamsikilizi, hamshirikishi mambo yake, sio mwaminifu, mkorofi n.k.

Pamoja na hayo yote mwanamke hupaswi kukata tamaa, hupaswi kuacha tu, unatakiwa kupambana, kusimama katika zamu yako, na kuomba kwa bidii. Ndoa nyingi zimesimama leo hii sababu ya ujasiri na moyo wa kutokukata tamaa wa nwanamke. Sio kosa lako mambo yamekuwa kama yalivyo, hivyo hakuna sababu ya kujilaumu bali Simama na Mungu, fanya yale ya nafasi yako na furahia maisha bila kuishi kwa unyonge kutokana na majaribu.

Mungu atakupa uwezo wa kuyashinda, Mungu atakupa mlango wa kutokea.

1 KOR. 10:13 SUV
“Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.”

Advertisements

3 thoughts on “Mwanamke Usikate Tamaa Katika Majaribu

  1. Amina Mtumishi.
    Mhh hasa jaribu la wadada wa kazi yani kwa kweli hatupaswi kukata tamaa ni kumwomba tu Mungu atusaidie.
    Ubarikiwe Mtumishi wa Bwana!

  2. Mungu atupe nguvu hasa jalibu la waume zetu kutoka nje ya kiapo cha ndoa Eeeh MUNGU tusaidie waja wako

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s