Mungu Bado ni Mungu Hata Nyakati za Shida

Wakati unapokuwa katika hali nzuri, mambo yako yanaenda kama ulivyopanga, kila kitu kwenye maisha yako kipo kwenye mstari, upo kwenye kilele cha furaha na mafanikio ni rahisi sana kuwatia moyo wengine, kukiri ukuu wa Mungu, kuongea maneno ya kuinua na kuamini kuwa Mungu atakuinua zaidi na zaidi. Ahadi za Mungu unaziona ni zako.

Lakini pale unapokuwa chini, kila unaloshika linafeli, mambo yako yote hayana muelekeo, kila upande ni madeni, magonjwa, shida na matatizo… Inakuwa Mungu sana kuliamini neno la Mungu. Ahadi za Mungu unaziona kama wewe zimekuruka. Unaona kama vile Mungu hayupo, amekuacha na hata mtu akikutia moyo unaona anaongea tu na yale uliyokuwa unayakiri mwanzo sasa unaona kama haiwezekani.

Nakutia moyo mpendwa, haijalishi hali gani unayopitia, Mungu bado ni mwaminifu na ni yeye yule hajabadilika kamwe. Mungu wa wakati wa raha bado ni Mungu hata wakati wa shida, Mungu aliyekufanikisha bado ni Mungu hata ukipita katika magumu, Mungu aliyewavusha wana wa Israel bahari ya shamu bado alikuwa Mungu  wakati wa vita. Hakika hatakuacha wala kukupungukia. Usiache kumuamini nyakati zote.

Advertisements

5 thoughts on “Mungu Bado ni Mungu Hata Nyakati za Shida

  1. Hakika MUNGU NI MUNGU aonekanaye wakati wa shida na raha,ukimtumainia yeye yote yawezekana haijalishi wapita katika Magumu ya kiasi gani Mungu ni yuleyule jana leo na hata milele.

  2. asante sana mpendwa kwa neno zuri la kuinua. Ni kweli Mungu hutuwazia mema daima na yote tunayopitia yatupasa kuutafuta uso wake na mapenzi yake ndani ya hayo. Mungu akubariki mno.

  3. mungu ni mwema hati mahali tunapodhani tumefika mwisho yeye huchukuwa usukani

  4. Mungu Wetu Ni Msaada Wakati Wowote, Tena Anatupatia Upendelea Hata Wakati Tunapopita Katika Bonde La Uvuli Wa Mauti

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s