Ukisalitiwa Mweleze Yesu

Hakuna jambo linaumiza kama kusalitiwa na mtu uliyempenda na ukamuamini mfano mzazi, mke, mume, mchumba, mtoto, kaka, dada au rafiki wa karibu. Maumivu yake huwa ni makali sana na huweza chukua muda mrefu sana kupona.

ZAB. 55:6-7, 12-13
“Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa, Ningerukia mbali na kustarehe.  Ningekwenda zangu mbali, Ningetua jangwani.  Kwa maana aliyetukana si adui; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo, ningejificha asinione.    Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana.”

Unaweza jaribiwa kurudisha kisasi au kumchukia huyo mtu kabisa. Lakini biblia inatukumbusha kuwa Yesu naye alijaribiwa kama sisi lakini hakutenda dhambi.

EBR. 4:15
“Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.”

Hivyo unapokuwa umesalitiwa na ndugu, mwendee Yesu yeye awezaye kuponya mioyo iliyojeruhiwa na kukupa moyo wa msamaha na kuachilia. Yesu alisalitiwa na mtu wake wa karibu, anajua maumivu ya usaliti na pekee ndiye awezaye kukuondolea maumivu hayo na kuuponya moyo wako. Usijaribu kutafuta suluhisho mwenyewe maana hutalipata, mkabidhi Yesu, lia mbele zake na hapo furaha yake itakuwa nguvu yako.

Advertisements

4 thoughts on “Ukisalitiwa Mweleze Yesu

  1. Ee Mumgu mwema tujaze roho wako mtakatifu ili tuweze kukuishia wew Kristo maisha yetu yote asante kwa fundisho lenye kujenga

  2. Jaman inauma sana na kilichoniuma sana juu ya kusalitiwa ni kwamba niliomba MUNGU anipatie mwenzi wangu wa maisha nikaoneshwa kijana mmoja ambaye alionesha nia hiyo miaka zaid ya kumi iliyopita then alipokuja tena niliomba zaidi na watumishi fulani tulienda vizuri kipindi tunapanga mikakati ya ndoa akaibuka mtu mlevi, mchafu na asiye na hofu ya Mungu akamchukua huyu niliyeamini alitoka kwa Mungu nikaachiwa majeraha nilibaki kumlilia MUNGU niliyemuomba mwenzi. Ni mwaka wa pili sasa sijapata mpenyo wa kumpat Mwenzi, INAUMA walau angekua ni mtu wa Mungu ndo kamchukua.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s