Kwa Kila Mke

Uko wapi ule upendo wako wa kwanza kwa mumeo. Kumbuka jinsi gani ulivyojaa furaha baada ya kijana uliyempenda kukuvalisha pete ua uchumba na kuja kwa wazazi wako kutoa mahari? Unakumbuka jinsi gani ulivyokuwa umejiandaa kumpenda na kumtii mumeo siku zote za maisha yako. Mwanzoni ulikuwa unaona raha kumhudumia mumeo na kumfurahisha lakini kwanini sikuhizi imekuwa ni kama msalaba kwako?

Chukua muda ufikirie jinsi gani ulikuwa unajibidiisha kupata muda wa kuwa na mwenzio siku hizi uko busy na watoto na marafiki basi. Ule upendo wa kummtendea mema kila siku umeenda wapi? Haijalishi amekuumiza kiasi gani, uliapa kumpenda, na hakika upendo hugeuza hata moyo wa chuma.

Kuanzia leo dhamiria kumtendea matendo ya upendo, kumuonyesha upendo hata asipostahili kabisa na utaona furaha itakavyozidi katika ndoa yako na amani kutawala daima. Upendo hufunika wingi wa dhambi na hauhesabu mabaya.

4 thoughts on “Kwa Kila Mke

 1. Hakika nampenda mume wangu achilia mapungufu yote aliyo nayo nampenda sana tena sana Mungu namwomba anizidishie upendo daima

 2. Women Christ

  Mpendwa nimesoma maelezo “statement” nimefurahi. Ukweli upendo wa mwanzo hukinzana sana na upendo endelevu.

  Sababu roho za ndani zinakuwa bado kushiba au kufahamu kwa nini ninakupenda. Kusema kweli ninampenda sana mume wangu japo siyo rahisi yeye kujua kama anapendwa.

  UPENDO wa DHATI.

  Lucy Mgilla

 3. Asante kwa fundisho nzuri. I will definitely make my marriage work no matter what. May the Almighty God help me. Amen

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s