Kwa Kila Mume

Kumbuka upendo wako wa kwanza kwa mkeo. Kumbuka yule binti uliyekuwa unakosa usingizi kwa ajili yake, ulivyokuwa unapita pita karibu na kwao ili walau umuone moyo wako utulie. Uliyekuwa huwezi kulala kabla hujaisikia sauti yake. Kumbuka jinsi moyo ulivyokuwa unadunda siku ya kwanza kumueleza ya moyoni na jinsi gani ulivyojaa furaha alipokubali kuwa nawe siku zote za maisha yako.

Je kwanini leo hii unamuona hafai tena? Leo hii msichana aliyekuwa mpenzi wa moyo wako unamtendea visivyo tena bila hata kujali? Je ule upendo wa kwanza umeenda wapi? Amka katika usingizi wako, huyo mkeo ndiye yule yule binti uliyekuwa huambiwi wala husikii juu yake, uliyeapa kumlinda, kumfurahisha na kuwa naye siku zote za maisha yako.

Chukua dakika chache ufikirie mwanzo wa penzi lenu, na pia andika kabisa vitu ambavyo ulikuwa unamfanyia na uso wake unachanua kwa furaha. Sasa azimia kuyafanya hayo yote kuanzia sasa. Hata kama kuna uzito ndani yako, jisukume kutenda na hakika hutajuta. Usiangalie amefanya nini na amekosa nini bali angalia ule upendo wako wa kwanza na dhamiria kuurudisha upya katika ndoa yako.

Nakwambia ukifanya hivi utakuja kunishuhudia jinsi furaha ya ndoa ilivyoongezeka mara dufu.

Advertisements

6 thoughts on “Kwa Kila Mume

  1. Ubarikiwe sana! Pamoja na mapungufu yake, Nampenda sana mke wangu! Mungu aniongoze katika hili.

  2. YAANI NINAPOSOMA HII: Kumbuka upendo wako wa kwanza kwa mkeo. Kumbuka yule binti uliyekuwa unakosa usingizi kwa ajili yake, ulivyokuwa unapita pita karibu na kwao ili walau umuone moyo wako utulie. Uliyekuwa huwezi kulala kabla hujaisikia sauti yake. Kumbuka jinsi moyo ulivyokuwa unadunda siku ya kwanza kumueleza ya moyoni na jinsi gani ulivyojaa furaha alipokubali kuwa nawe siku zote za maisha yako.Je kwanini leo hii unamuona hafai tena? Leo hii msichana aliyekuwa mpenzi wa moyo wako unamtendea visivyo tena bila hata kujali? Je ule upendo wa kwanza umeenda wapi? Amka katika usingizi wako, huyo mkeo ndiye yule yule binti uliyekuwa huambiwi wala husikii juu yake, uliyeapa kumlinda, kumfurahisha na kuwa naye siku zote za maisha yako.Chukua dakika chache ufikirie mwanzo wa penzi lenu, na pia andika kabisa vitu ambavyo ulikuwa unamfanyia na uso wake unachanua kwa furaha. Sasa azimia kuyafanya hayo yote kuanzia sasa. Hata kama kuna uzito ndani yako, jisukume kutenda na hakika hutajuta. Usiangalie amefanya nini na amekosa nini bali angalia ule upendo wako wa kwanza na dhamiria kuurudisha upya katika ndoa yako.Nakwambia ukifanya hivi utakuja kunishuhudia jinsi furaha ya ndoa ilivyoongezeka mara dufu.NINAIPENDA NA INANIPA MOYO SANA. MUNGU AENDELEE KUWATUNZA MZIDI KUELIMISHA.

    From: Women Of Christ To: rmasawen@yahoo.com Sent: Thursday, October 16, 2014 10:52 AM Subject: [New post] Kwa Kila Mume #yiv7335155013 a:hover {color:red;}#yiv7335155013 a {text-decoration:none;color:#0088cc;}#yiv7335155013 a.yiv7335155013primaryactionlink:link, #yiv7335155013 a.yiv7335155013primaryactionlink:visited {background-color:#2585B2;color:#fff;}#yiv7335155013 a.yiv7335155013primaryactionlink:hover, #yiv7335155013 a.yiv7335155013primaryactionlink:active {background-color:#11729E;color:#fff;}#yiv7335155013 WordPress.com | womanofchrist posted: “Kumbuka upendo wako wa kwanza kwa mkeo. Kumbuka yule binti uliyekuwa unakosa usingizi kwa ajili yake, ulivyokuwa unapita pita karibu na kwao ili walau umuone moyo wako utulie. Uliyekuwa huwezi kulala kabla hujaisikia sauti yake. Kumbuka jinsi moyo ulivyok” | |

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s