Mungu Hatakuacha

Unapopitia magumu na mambo ya kukatisha tamaa wakati mwingine unaona kama Mungu amekuacha. Yesu alipokuwa msalabani alipitia hali hiyo, na Ayubu katika majaribu magumu alipitia pia hali ya kukata tamaa na kuona kuwa Mungu amemuacha.

MT. 27:46
“Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
AYU. 13:24
“Mbona umeuficha uso wako, Na kunihesabu kuwa ni adui yako?”

Maumivu makubwa ya moyo lazima yataleta simanzi na kukata tamaa. Lakini hatupaswi kwenda huku na kule kuuliza kwa watu kwanini tunapitia hayo bali tumwendee Mungu, muulize yeye maswali yote na hakika atakuonyesha ni kwanini ameruhusu upitie hayo. Baada ya majaribu magumu Mungu alimuinua Yesu na kumfanya juu ya vyote, na baada ya Ayubu kushinda Mungu alimzidishia mara dufu ya yale aliyoyapoteza.

Unapokuwa huelewi, usitafute jibu kwa wanadamu bali kwa Mungu na ameahidi hatakuacha wala kukupungukia.

EBR. 13:5b
“kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.”

Advertisements

3 thoughts on “Mungu Hatakuacha

 1. naomba nami nijiunge na maombi ya usiku,penetration yangu sitaweza
  namba yangu ya siku 0762681111

 2. BWANA YESU ASIFIWE! MIMI NI MAMA WA MTOTO MMOJA ,NIPO KATIKA NDOA NI MWAKA WA 5 SASA LAKINI NDOA YANGU HAINA AMANI,HAKUNA UPENDO ,SITHAMINIKI SI MME WANGU SI FAMILIA YAKE HAWANITAKI.IMEFIKA MDA NATAMANI KUONDOKA. MME WANGU HAJAOKOKA ILA MIMI NIMEOKOKA.NAHITAJI MSAADA WA MAOMBI NA USHAURI PIA KWAKUWA KUNA MDA NAKATA TAMAA.NIMEMLILIA MUNGU MIMI NA WAZAZI PAMOJA NA NDUGU LAKINI HAKUNA MAJIBU. SIKUWAHI KUTAMANI TALAKA NA WALA KUVUNJA NDOA YANGU LAKINI KHALI INAZIDI KUWA MBAYA.

 3. Joyceline Moshy Says:
  Naomba nimshauri dada Rehema kuwa asikate tamaa hata kidogo. Pale anapofikia njia panda ndipo Mungu anapotenda. Kumbuka kuwa huyo ni mume wako mliahidi madhabahuni mbele ya Mungu na mashahidi wengine.
  Wakati mwingine inakubidi utubu pia kwa ajili yake na familia yake, aidha angalia kama kuna mahali ulianguka nawe utubu ili Mungu amkomboe mume wako.
  Funga na kuomba kwa ajili yake ombea hata vitu vyake kama nguo hadi za ndani maana ibilisi huwa nakamata sana wanaume walioko kwenye ndoa. Mpende zaidi na zaidi badilisha mwenendo wako hata wa maombi.
  Naamini kabisa Mungu wetu ni mwaminifu sana na anaangalia uaminifu wako kwake. hao wazazi wake pia wapende sana wala usionyeshe chuki yoyote ilishetani akose cha kukushtaki.
  Mungu akubariki sana mama usikate tamaa wanawake ni walinzi wa waume zao.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s