Heri ya Mwaka Mpya

Happy New Year Watu wa Mungu. Mungu wetu ni mwaminifu sana, anastahili sifa na shukrani kwa yote aliyotutendea kwa mwaka mzima. Jina la Bwana libarikiwe!

Nikutie moyo rafiki yangu, inawezekana mwaka jana ulikuwa mwaka wa mapito sana kwako. Mipango yako mingi haikufanikiwa, kila kitu kilienda sivyo na umefika mahali umekata tamaa hata ya kuweka malengo tena. Kama tulivyoona juzi kuwa baada ya mapito Ayubu aliinuliwa na Mungu na kuvuka kwa ushindi, nawe pia Bwana atakuinua na kukuvusha.

Haijalishi miaka mingapi imepita, mipango mingapi imeharibika, Mungu wa Israel yupo kuihuisha tena na kukuinua zaidi na zaidi.  Ayubu naye alipitia hali ya kukata tamaa, kuona kuwa makusudi yake hayapo tena
AYU. 17:11
“Siku zangu zimepita, makusudi yangu yamevunjika, Hata hayo niliyo nayo moyoni mwangu.”

Lakini Mungu hakumuacha, Mungu alimpa tena kusudi la kuishi, Mungu alimbarikia zaidi na zaidi.
Inuka, jitie nguvu ndani ya Yesu.. tembea kwa ushindi maana Bwana wa mabwana yu ndani yako. Yeye ni Immanuel Mungu pamoja nasi..

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s