Furaha ya Bwana ni Nguvu Yetu

NEH. 8:10b
“maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.”

Furaha ya mambo ya dunia hii ni ya muda mfupi sana na kamwe haiwezi kuwa nguvu yako wakati wa matatizo. Ni furaha isiyodumu na isiyoondoa hofu. Ni furaha yenye mwisho.

Utafurahi sana siku umefaulu mtihani lakini baada ya muda mfupi utaanza kuhuzunika hajapata kazi.
Utafurahi sana siku ukipata kazi lakini baada ya muda mfupi utahuzunika kazi ngumu, bosi anakunyanyasa, wenzio hawakupendi n.k
Utafurahi sana siku unafunga ndoa lakini baada ya muda unaanza kuhuzunika mwezi wako anakiburi, mkali, mlevi, au anachepuka.
Utafurahi sana umepata mtoto lakini utaanza kuhuzunika siku akiugua au akifanya tofauti na ulivyomfundisha.

Yani hapa ni kwauchache tu tunaona ambavyo furaha ya mambo ya duniani ni ya muda mfupi. Lakini furaha ya BWANA ni nguvu yetu na ni ya kudumu. Efeso 4:4. Katika yote hayo hapo juu na mengine mengi furaha ya BWANA pekee ndio itakufanya kuendelea mbele kwa ushindi bila kuwa mtu wa huzuni siku zote. Usitegemee furaha katika mambo ya dunia bali toka kwa Mungu pekee. Usihuzunike kwa yale unayoyapitia bali furahi katika Bwana siku zote maana furaha ya Bwana ni nguvu yetu.

Advertisements

3 thoughts on “Furaha ya Bwana ni Nguvu Yetu

  1. MUNGU AKUBARIKI MTUMISHI WA MUNGU KWA MAFUNDISHO MAZURI SANA JINA LA BWANA LIBARIKIWE SANA NAOMBA UNIOMBEE NIWE NA FURAHA YA BWANA SIKU ZOTE AMEN

  2. NAOMBA SANA MAOMBI YAKO FAMILIA YANGU IWE NA FURAHA YA BWANA YESU KRISTO AMEN

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s