Simama na Mungu kwenye Ndoa Yako

Wapendwa leo nimejisikia kuongea na wanandoa wote. Maadamu uliamua mwenyewe kuolewa, mumeo ulimpenda bila kulazimishwa na una Roho mtakatifu kamwe usinene mabaya juu ya ndoa yako wala kuikatia ndoa yako tamaa. Ni ukweli usiopingika kuwa kwenye ndoa utapita hatua mbalimbali, utapanda milima na kushuka mabonde na utalia na kucheka lakini mwisho wa siku lazima iwe ushindi.

Kuna matatizo yatatokea ndani ya ndoa sababu ya tofauti zenu, mengine sababu ya ujinga na kutokuelewa na mengine ni shetani kwa 100% maana hayana maelezo. Katika yote hayo msingi wa ushindi ni maombi, kuchukuliana na kusamehe. Mambo haya matatu ni msingi mkuu sana wa ndoa yako. Kamwe usiruhusu kiburi, kisasi au kinyogo kuchipuka ndani ya ndoa yako. Haijalishi mwenzio amekosea kiasi gani na haijalishi ameomba msamaha au la..una jukumu la kumuombea, kumchukulia na kumsamehe na juu ya yote kumtii. Pale unapoona panahitaji kuongea kaa naye muongee mfikie muafaka.

Usipende kabisa narudia usipende kabisa kutatua matatizo yako na mumeo kwa kumwambia mtu mwingine. Jitahidi kujifunza kuongea na mumeo hadi kufikia muafaka ili mambo ya ndoa yenu yawe yenu wawili tu. Mwingine ni Mungu. Kila unapomzungumza mumeo mzungumze kwa mema na sifa kede kede mengine mapungufu mwambie Yesu. Maneno huumba so jenga tabia ya kumsema vizuri mumeo kuanzia ukiwa mwenyewe hadi mbele za watu. Mheshimu mumeo hata unapokuwa mwenyewe yani mawazoni mwako.

My dear ndoa ukiyonayo ndio hiyo hiyo hakuna kubadili wala kuanza upya so una kila sababu ya kuhakikisha inakuwa yenye furaha na amani no matter what. Hata pale unapoona kama it will never be jua kuwa it will be na usikate tamaa kabisa. Kwa miaka yangu 9 ya ndoa nimeona mengi na kupitia mengi na katika yote nimejifunza we can choose to be happy or to dwell in the negatives. Si kwa uweza wala nguvu bali ni kwa Roho wa Mungu. Tuna msaidizi ambaye yupo nasi kila mahali, msaidizi anayetafuta kutuona wenye furaha daima. Msaidizi ambaye yupo kukusaidia katika kila eneo kwenye ndoa yako.

Advertisements

11 thoughts on “Simama na Mungu kwenye Ndoa Yako

  1. Amen and Amen. Natamani somo hili liwafikie wengi, maana sisi wanawake tuna nafasi kubwa sana katika kujenga au kubomoa ndoa zetu.

  2. Nashukuru sana kwakutukumbusha wajibu wetu katika ndoa zetu Mungu atusaidie maana shetani naye yuko kazini akikazana kutuvuruga ili tusiweze kutimiza mpango mzima wa Mungu katika maisha yetu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s