CHALLENGE : SIKU 30 ZA KUMTIA MOYO MUME- SIKU YA TATU

Upendo huvumilia, hufadhili; Upendo huona zaidi ya mapungufu. Inawezekana kabisa kuna mambo unatamani mumeo ayafanye kwa namna fulani ndio utafurahi ila unaona kabisa yeye hafanyi hivyo na ni kama hataki. Mfano unatamani kila siku awe anakaa na wewe na kusikiliza kila tatizo lako na kujadili na wewe ila yeye anakuwa busy na mambo mengi hivyo hakupi muda wa kutosha; unatamani muwe mnatoka pamoja mara kwa mara ila yeye anapendelea zaidi kukaa nyumbani na kupumzika; inawezekana kuna mambo unatamani ayafanye kwa namna fulani ila yeye anafanya kwa namna nyingine. Badala ya kulalamika kama ulivyozoea, leo mshukuru kwa lile analofanya na ufunge macho kwa lile ambalo unaona amekosea. Mpende na mkubali jinsi alivyo na mfurahie. Pale anapotaka kukusaidia jambo fulani usimlazimishe afanye kama unavyotaka wewe, kubali ‘uniqueness’ yake na uifurahie.

Huwezi kutarajia mumeo ndio awe jawabu la mahitaji yako yote ya kihisia (furaha ya kweli, amani, tumaini) haya yote anayeweza kukupa kwa ukamilifu ni Mungu pekee. Mruhusu autawale moyo wako na hakika utamfurahia mumeo.

Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
1 KOR. 13:4

womenofchrist.wordpress.com

Advertisements

One thought on “CHALLENGE : SIKU 30 ZA KUMTIA MOYO MUME- SIKU YA TATU”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s