Yesu Anakupenda Sana

Yohana 3: 16-17Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”

Mungu anakupenda sana, anajua jinsi unavyoenenda na amemtuma Mwana wake wa pekee, Yesu afe msalabani kwa ajili ya ukombozi wako. Haupaswi tena kuendelea kuishi dhambini, neema ya wokovu imefunuliwa na yapatikana bure kwa kumkiri na kumwamini Yesu.

Warumi 10: 9-10 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”

Amua leo kumpa Yesu maisha yako upate tumaini jipya la uzima wa milele. Ukimpokea Yesu utapata furaha, amani na uzima wa kweli. Huwezi kuzipata baraka za Mungu kama hauna ushirika naye, na pia huwezi kushinda dhambi bila msaada wa Mungu. Kama upo tayari kumpa Yesu maisha yako, sali sala hii kwa kumaanisha kutoka moyoni.

“BWANA Yesu, nakuja mbele zako mimi ni mwenye dhambi. Nimetambua makosa yangu na kuwa siwezi peke yangu. Naomba uingie ndani ya moyo wangu, uondoe kiu ya dhambi, unisamehe makosa yangu yote, ufute jina langu kwenye kitabu cha mauti, na uliandike kwenye kitabu cha uzima. Nimeamua kukufuata wewe na kujitoa kwako siku zote za maisha yangu. Nisaidie niweze kutembea nawewe daima.”

Hongera! Sasa umeokoka. Tafuta kanisa linalohubiri kweli ya neno la Mungu uwe mshirika hapo. Jifunze biblia na omba kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu.

Advertisements

10 thoughts on “Yesu Anakupenda Sana

  1. nimevutiwa sana na mafundisho yako dada nahitaji kumjua YESU zaidi maana ndiye bwana na mwokozi wangu. Barikiwa mtumishi wa mungu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s