Lishe ya Mtoto: Miezi 6-12

Kwa miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto chakula pekee ambacho wataalamu wa afya wanashauri apewe ni maziwa ya mama tu. Kunyonyesha ndio njia ya kwanza kabisa kumpa mtoto chakula. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo wakati ana miezi michache utoaji wako wa maziwa unaathirika maana jinsi mtoto anavyonyonya ndivyo jinsi maziwa yanavyotengenezwa ndio maana watu wengi wanavyoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao yanaanza kupungua. Faida za kunyonyesha maziwa ya mama ni pamoja na:

  1. Maziwa ya mama yana virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa mtoto. Humlinda na magonjwa mengi ya utoto pamoja na ‘allergies’ mbalimbali.
  2. Hukuwezesha kuwa na ukaribu na mtoto wako.
  3. Hukupunguzia uwezekano wa kupata kansa ya matiti.
  4. Ni bure na unaweza kumpatia maziwa wakati wowote bila usumbufu.

Wakati gani Uanze Vyakula Vingine

Mtoto wako akifikisha miezi 6 unaweza kuanza kumpatia vyakula vingine kidogo kidogo ( Kuna ambao kutokana na sababu Fulani daktari huwashauri kuanza mtoto akiwa na miezi 4 hivyo ni  vyema ukiwasiliana na daktari wako kwanza). Mtoto akianza kupewa vyakula nje ya maziwa mapema kabla ya miezi 4 ni hatari kwa afya yake maana mfumo wake wa kusaga chakula unakuwa bado haujawa tayari. Unapoanza kumpa vyakula vingine hauachi kumnyonyesha, unyonyeshaji unaendelea hadi miaka miwili na nusu.

Dalili kuwa mtoto wako yupo tayari kuanza vyakula vingine ni:

  1. Amefikisha miezi 6
  2. Anaweza kushikilia kichwa juu ( shingo imekaza)
  3. Anaweza kukaa kwa kuwekewa kitu ( mfano kiti chenye mkanda)
  4. Unapompa chakula na kijiko anafungua mdomo kutaka kupokea au anageuza uso kwa kukataa
  5. Akipokea chakula anakiweka mdomoni na kujaribu kumeza na sio kukisukuma nje na kuacha mdomo wazi.

Hakikisha mtoto wako yupo tayari kabla hujaanza kumpa chakula na usimlazimishe sana anapoanza maana anaweza kuchukia chakula, inawezekana hapendi chakula ulichompa jaribu kubadilisha uone anapenda nini. Kila mtoto ni tofauti na mwingine hivyo usimlinganishe mtoto wako na mwingine la muhimu ni kuhakikisha kuwa anauzito kulingana na umri wake na anaongezeka kwa kupanda chati.

Mnapokuwa mnakula mezani mtoto naye awe hapo ili kumpa hamu ya kula na sio kila wakati akila anakuwa peke yake. Mpe chakula akiwa na furaha na pia akiwa na njaa ili aweze kufurahia chakula chake. Kabla ya kubadilisha aina ya chakula mpe kwa siku 3-4 mfululizo ili aweze kukizoea na kama kitamletea madhara ujue hasa ni chakula gani. Usimchanganyie vyakula maana hutajua anapenda nini na kuchukia nini na pia kama kuna kitu kitamdhuru ukichanganya hautagundua kwa urahisi.

Miezi 6-9

Endelea kunyonyesha na anza kumpa vyakula vyenye madini ya chuma. Mtoto alishwe kwa ratiba inayoeleweka kila siku na katika ratiba hiyo hakikisha angalau mara moja kwa siku muda wake wa kula unakuwa sawa na muda wa familia yote ili muweze kula pamoja. Vyakula vyake viwe vimepondwapondwa kabisa ikiwezekana tumia blender na hakikisha anapata mlo kamili yani matunda, mbogamboga, mbegu, nafaka, nyama na samaki. Inashauriwa kutokuchanganya aina tofauti za nafaka kwenye unga mmoja unapomtengenezea uji, uwe na unga wa mahindi, ulezi,mchele n.k tofauti tofauti. Pika aina moja ya uji kwa wakati unaweza kufanya kwa wiki au vyovyote utakavyopenda.

 Unapompa mboga au matunda anza na tunda moja moja kwa wakati. Osha vizuri matunda yako na katakata vizuri na kuponda ponda kisha mpe kiasi kidogo kwa wakati na kikibaki usikiweke, mtengenezee kile atakachokula tu. Matunda kama papai, parachichi na embe ni mazuri kwa kuanzia. Chemsha maharage, njegere au mboga za majani na kumpa supu kidogo kidogo, usiweke chumvi nyingi kidogo sana inatosha. Usimpe juisi za madukani, hakikisha unamtengenezea juisi wewe mwenyewe na usichanganye matunda mbalimbali kwenye juisi moja, na usiweke sukari kabisa.

Miezi 9-12

Katika umri huu mtoto anakuwa tayari amezoea ladha tofauti tofauti za vyakula mbalimbali nje ya maziwa. Anauwezo wa kukaa na kushikilia kitu kwa mikono yake na kuweka mdomoni hivyo anza kumpa matunda laini mkononi aanze kujifunza kula mwenyewe. Hakikisha vipande sio vidogo sana anavyoweza kumeza ili kuepuka hatari ya kukabwa. Kwa sababu pia atakuwa ameanza kuota meno atakuwa anapenda sana kutafuna tafuna. Katika umri huu pia unaweza kuanza kumpa kiini cha yai, ute wa yai hadi afike umri wa mwaka mmoja. Endelea kumnyonyesha ila kwa sasa anakula kwanza kisha ndio ananyonya maana akinyonya sana anaweza akakataa chakula. Usimpe chakula kimoja mfululizo kwa muda mrefu maana atakinai na kuanza kukataa chakula, mpe vyakula tofauti tofauti ili aendelee kupenda chakula.

Jinsi ya Kutengeneza Chakula cha Mtoto

Ni rahisi sana kutengeneza chakula cha mtoto nyumbani kwako. Osha mikono yako vizuri kabla ya kuandaa chakula na hakikisha unatumia vyombo visafi.

Matunda na mboga mboga: osha mboga zako vizuri kwa maji safi ( ya uvugu vugu) na kisha katakata na kubandika jikoni kwa chumvi kidogo sana bila mafuta. Ikichemka isage kwenye blender au ponda ponda iwe laini kabisa kisha mpe mtoto. Matunda osha pia kwa maji ya uvugu vugu, toa ganda la nje na kata vipande vikubwa kama unataka ale kwa mikono yake mwenyewe au ponda ponda na upe kwa kijiko.

Nyama na Samaki: Chemsha vipande vya nyama na maji kidogo na iive kwa moto wa kiasi hadi ilainike kabisa kisha isage kwenye mashine (food processor) na umpe na ile supu. Samaki vile vile ila samaki hakuna haja ya kuisaga maana ikiiva inalainika sana na ni rahisi kwa mtoto kula bila taabu (Kuwa makini sana na mifupa!).

Mbegu: Hapa nazungumzia maharage, kunde, choroko, njegere n.k Pika hadi ziive kabisa na kulainika kisha pondaponda na kumpa mtoto. Pia viazi na ndizi vinafaa sana kwa watoto, unaweza ukachanganya na supu ya samaki / nyama au na maziwa.

Nafaka: Usichanganye nafaka tofauti tofauti kwa ajili ya uji wa mtoto, inashauriwa kuwa na unga tofauti kwa kila nafaka. Unapopika uji unaweza kuweka karaga zilizosagwa ili kuongeza mafuta na vitamin kwenye lishe ya mtoto.

Usalama katika Kula

  1. Hakikisha haumuachi mtoto mdogo na chakula au kinywaji bila uangalizi hata kama ni maziwa ya chupa asije akapaliwa. Usimpe mtoto chakula au maziwa akiwa amelala, analia au anacheka.
  2. Usimpe chakula ambacho kinaweza kumkaba au kumpalia kama karanga, maindi, zabibu n.k
  3. Kabla ya kumpa mtoto chakula hakikisha umekiangalia joto lake usije ukamuunguza mdomo.
  4. Usafi wa mtayarishaji, mlishaji na mlishwaji ni muhimu san asana.

Mfano wa Ratiba ya Mlo wa Mtoto

Ratiba hii ni ya mfano tu, vyakula vilivyotenganishwa na / inamaana nikimojawapo kati ya hivyo. Hakikisha vyakula havichukui nafasi ya maziwa maana ni ya muhimu kwa afya ya mtoto wako.

MUDA MIEZI 6 – 9 MIEZI 9 – 12
Alfajiri (saa 11-12) Maziwa ya mama Maziwa ya mama
Asubuhi (saa 1-2) Maziwa ya mamaUji ( Cerelac)

Tunda la kupondwa pondwa

Maziwa ya mamaUji ( Cerelac)

Tunda la kupondwa pondwa

Kabla ya mchana (saa 4-5) Maziwa /  Kipande cha mkateMaji Maziwa / andazi / chapatti laini / Kiini cha yaiMaji
Mchana (saa 6-7) Ndizi / Viazi / Wali vya kupondwa pondwaSupu ya mboga ya majani / mbegu / samaki / nyama

Tunda la kupondwa pondwa

Ndizi / Viazi / Wali / UgaliMboga za majani / Nyama / Mbegu / Samaki

Kipande cha Tunda

Alasiri ( Saa 9-10) Maji Maji
Jioni (saa 12-1) Uji / CerelacSupu ya mboga / mbegu / nyama / samaki Uji / CeleracMboga / Mbegu / Nyama / Samaki
Usiku ( muda wowote) Maziwa Maziwa

320 thoughts on “Lishe ya Mtoto: Miezi 6-12

  1. Nimependa hilo somo,nina mtoto anakaribia kufikisha miezi sita.Kwa nini umesema sio vizuri kuchanganya nafaka kwa ajili ya kumtengenezea uji?kuna sababu yeyote ya kiutaalamu ninaweza kuifahamu?asante

  2. Kuna daktari wa watoto alinielimisha kuhusu jambo hili, sababu kama utaanza kumchanganyia mtoto nafaka na mtoto wako ana aleji na nafaka mojawapo hutajua itakuwa ngumu kugundua jambo hilo pia kama mtoto wako hapendelea nafaka fulani utazidi kumlazimisha kunywa uji kumbe hapendi ulezi au mahindi au mtama n.k. Kama unahitaji kumchanganyia hakikisha kabla ya kufanya hivyo umempa uji wa nafaka moja kwa wiki nzima mfululizo ili kama kuna tatizo uweze kuligundua kwa urahisi na baada ya hapo utajua nini umchanganyie na nini usimchanganyie. Epuka kuchanyanya nafaka na mazao ya jamii ya kunde maana mazao ya jamii ya kunde huchelewa kuiva hivyo kunahatari ya kumathiri mtoto kama ukipika kama uji wa kawaida.

  3. Mungu awabariki sana kwa kutuelimisha.mimi mwanangu ana miezi nane je naweza mtengenezea juisi za aina gani nzuri kwake?Ahsanteni sana.

  4. I love this site its very educative. Please update me each time you have new things.

    Florence from Kenya a Nutritionist

  5. Tunakushukuru sana dada kwa kuendelea kutuelimisha.

    Jamani mimi nina mtoto wangu anasumbuliwa na kifua, nimempeleka hospital kapewa dawa zote za kifua, kinakuwa kama kinaiva anaanza kubanja, kabla hajapona kinarudia tena, nisaidieni jamani nimpatie nini?

    nimeambiwa nikung’ute vumbi, nimefanya hivyo lakini si unajua tena vumbi la hapa kwetu bongo.

    lakini nimejifunza kitu hapo juu, hivi ni kweli uji wa ulezi unaweza kumsababishia kifua? manake ameshaanza kunywa uji.

    ana miezi sita namchanganyia ulezi na mahindi.

  6. Helo judith,
    matatizo ya kifua kwa watoto yanaweza kutokana na sababu nyingi ikiwemo vumbi, kuwa kwenye baridi bila kufunikwa vizuri hasa kichwa, miguu na kifua, kukaa na nguo iliyolowa jasho, feni na mengine yakuzaliwa nayo au alergies ya paka, majani fulani n.k. Nakushauri mpeleke kwa daktari specialist wa watoto huku utapata matibabu ya kumfaa.
    Be blesed

  7. Nashukuru sana dada, nilienda kwa Dr. Hameer pale Fire ndo kanambia mambo ya vumbi baada ya kunibadilishia dawa zaidi ya mara 5, mwisho nikaenda kwa Dr. bale Dar Group ya pale tanda mti yule alinipa dawa ndo ikamsaidia kukiivisha akaanza kubanja na kupunguza kukooa lakini mpaka sasa hivi bado anakooa japo si sana. Mshauri mwingine alinambia labda ulezi unaweza kumsababishia nimemuachisha nampa uji wa mahindi tu. simvalishi kofia sababu sasa hivi ni joto na mwanangu anatoka jasho sana. labda kama mnamfahamu Dr. mwingine specialist wa watoto nisaidieni nimpeleke. sasa hivi usiku ndo anakooa akistuka tu lazima akooe.

  8. Nimekuelewa Judy
    Kuna daktari specialist wa watoto anafanya kazi muhimbili ila ana hospitali yake morroco anaitwa Dr masawe jaribu kumpeleka huko maana Dr huyu ni professor wa magonjwa ya watoto.
    ubarikiwe.

  9. Asante sana kwa somozuri mimi nina mtoto ana miezi nane bado ni mregevu ndio anaonyesha dalili za kukaa shingo limekaza sana naomba ushauri tafadhali

  10. Dada hongera kwa kutufungua macho na tena Mungu akujalie uzidi kutuelewesha. mie mwanangu jamani anakifua kila akitaka kula ama akiona chakula anakohoa jaman nimempa dawa ya minyoo lakini wapi?

  11. Nakusalimu mama Trinity, tafadhali naomba unitumie reading material za jinsi ya kumuosha mtoto mchanga na jinsi ya kujitunza kwa mama aliiyejufungua kwa njia ya upasuaji{ c-section}. Thanks alot

  12. Ubarikiwe sana mpendwa, ninajua Mungu atakulipa kwa jinsi unavyojitoa kwa ajili ya wengine.Kama kuna jambo lingine usisite kutufundisha.

  13. ubarikiwe mpendwa kwa ushauri mzuri kuhusu lishe ya mtoto.ila je kama mtoto hapedi kula unasaidiaje?tadhali naomba ushauri wako, mtoto wangu anamwaka mmoja na miezi miwili ila hapendi kula.

  14. Nimekuwa busy kidogo na kusahau kuhusu maswali yako, nitakutafutia na kuyaweka hapa soon. By the way naitwa mama kenneth na sio mama trinity

  15. shalom
    watoto wengi katika umri huo huwa hawapendi kula na mara nyingi hutokana na kutaka kao kuwa independent hivyo hawataki kupewa amri yoyote wala maelekezo bali wafanye wanavyotaka wao. nitakueleza kwa kirefu nini cha kufanya. Ubarikiwe

  16. nina mtoto wa kike nampenda sana ana mwaka 1 na miezi 5 ila hapendi kula kabisa. yeye anapenda kunywa maji tu hata kunyonya hataki. anatumia maziwa ya ng’ombe wakati nikiwa kazini nikirudi anaendelea na ziwa langu. je nitumie njia gani ili aweze kula? naomba msaada wako

  17. nina mtoto wa kike nampenda sana ana mwaka 1 na miezi 5 ila hapendi kula kabisa. yeye anapenda kunywa maji tu hata kunyonya hataki. anatumia maziwa ya ng’ombe wakati nikiwa kazini nikirudi anaendelea na ziwa langu. je nitumie njia gani ili aweze kula? naomba msaada wako.

    tatizo jingine anasumbuliwa na kifua mara kwa mara anakohoa sana nampa dawa kinafikia kubanja baada ya hapo kinarudia tena. nifanyeje

  18. Dada Agness, kwa swala la kifua ni vizuri ukamuona daktari kwa vipimo zaidi huenda kuna tatizo ambalo bado hujaligundua. Kuhusu watoto kukataa kula hili ni tatizo la watu wengi sana na nimeona sitaweza kujibu mwenyewe kwa uzoefu hivyo natafuta mtaalamu wa kutusaidia katika hili hivyo endelea kuvumilia kidogo.
    Ubarikiwe

  19. Ni kweli unachosema, tatizo linakuja kwenye kliniki zetu mnakuwa wengi kiasi kwamba nesi hawezi kupata muda wa kuongea na mzazi mmoja mmoja. Ni vyema tukawa na kawaida ya kuwapeleka watoto kwa daktari wa watoto kwa check up hata kama hajaugua na pale anapougua usimpe dawa bila kumpeleka kwa daktari.

  20. please send me materials for effects of not attending clinic for the baby in kiswahili

  21. Mungu akubariki sana dada. Nimejifunza kitu kizuri sana. Hata mimi Juzi nilimpeleka mtoto kwa daktari akanieleza hili la kuchanganya nafaka nyingi kwenye uji wa mtoto mchanga, akanielekeza niwe na nafaka tofauti tofauti ili niwe nambadilishia,hii inasaidia hata mtoto asikinai uji.

  22. Shalom,
    nimefurahishwa sana na mada hii hapo juu ila mimi ni mfanyakazi na nikitoka alfajiri hurudi jioni mtoto wangu wa miezi miwili na nusu naweza kumwanzishia uji au maziwa labda?

  23. samahani kwa kuchelewa kukujibu nilikuwa mgonjwa mpendwa. Kuhusu kumuanzisha mtoto uji, hapana haishauriwi kabisa katika umri huo maana tumbo lake bado halijawa na uwezo wa kupokea vitu zaidi ya maziwa. Unaweza kukamwanzishia maziwa ya formula ya watoto, ya ngo’ombe kama una mtu anayeamninika au unaweza kuwaona wataalamu wa afya wakuelekeze namna ya kukamua ya kwako na kumhifadhia unapokuwa kazini.

    Mungu akubariki sana

  24. hallow mama mimi nina mtot wa miezi 7 nilimzaa akawa na matatizo ya kushindwa kupumua akawekewa oxygen almost two week.mpaka sasaafya yake anenepi uzito anaongezeka kidogodogo najitaidi kumpa vyakula mbalimbali lakini hakuna.ngozi yake inakuwa kavu ikabidi nimpeleke kwa specialist wa ngozi muhumbili akasema ana pumu.sijui nifanyaje jamani mwanangu ata anenepi kabisa anaonekana mdogo.naomba ushauri mama yangu,nitamsadiaje mimi mwenyewe maziwa yangu yanatoka kwa shida ni mfanyakazi na nilimuanzishia maziwa ya lactogen nimejaribu kumpa maziwa ya ngombe naona anatoka vipele mkononi.nishauri mama yangu

  25. dada Lisa
    Mtoto wako anahitaji kuonana na daktari mahususi wa watoto, mpeleke kwa daktari wa watoto ili aweze kukupa ushauri wa kitaalamu na tiba kutokana na tatizo la pumu linalomsumbua.

  26. Ubarikiwe mama kwa huduma ya kuelimisha jamii.
    Nimekipata nilichokuwa nahitaji.
    God Bless u.

  27. asante sana kwani makala yako imekuwa msaada kwangu. mwanangu kafikisha miezi sita ila nilikuwa sijui ntakuwa nampa chakula kwa ‘interval’ gani. mungu akubariki, endelea kutuandikia makala nzuri za kutuelimisha.

    ushauri wa bure kwa wamama wenzangu ni kuwa tupende kufuata ushauri wa kitaalam kuhusu lishe za watoto wetu na sio kufanya mambo kienyeji. wengi wanadharau ushauri wa kitaalam hivyo utakuta anamuanzishia mtoto chakula kingine kabla ya miezi sita.

    binafsi mwanangu hajanywa forumulas tangu azaliwe, si kwamba nashinda nae masaa yote, no ila huwa namkamulia namuachia. nilipata ushauri toka kwa mtaalam jinsi ya kuyakamua, kuyahifadhi na kiwango cha kumpa.

  28. Kwanza nashukuru kwa ushauri wako wenye msaada mkubwa sana kwangu. Naomba kufahamu Cerelac ni nini na ina manufaa gani kwa mtoto? Jaman nisaidien kuuliza sio ujinga!

    Ubarikiwe

  29. Karibu mama jessy
    cerelac ni chakula cha watoto kinachotengenezwa kwa kutumia ngano, maziwa, wakati mwingine na flavour za chocolate na ndizi ambacho kipo tayari toka kiwandani unakichanganya na maji ya moto kutokana na kipimo kilichoainishwa na kumpa mtoto kama uji. Mara nyingi wazazi hutumia pale wanapokuwa mbali na nyumbani na hawawezi kubeba uji, safarini na hata nyumbani. Ni chakula chenye lishe na kunachoboresha afya ya mtoto. cerelac inapatikana madukani na ni kwa mtoto anayeanzia umri wa miezi 6.

  30. Habari za leo!
    tafadhali naomba kujua, nifanyeje ili mtoto wangu aendelee kunyonya maziwa ya mama, sababu ni mdogo sana ana miezi saba tu ghafla amekataa kunyonya maziwa yangu nami ningependa ni mnyonyeshe angalau kwa muda miaka miwili lakini sasa hataki kunyonya ana nyonya vidole vyake. je nifanyeje????

  31. Mtoto akikataa kunyonya ziwa la mama ni ngumu sana kumlazimisha kulirudia. Jaribu kumuacha kwa muda wa siku moja au mbili kisha mjaribu tena, akikataa jaribu kuonana na mtaalamu wa afya labda anaweza kukusaidia. mtoto wangu alikataa katakata akiwa na miezi 6 hivyo ikanilazimu kutafuta lishe na maziwa mbadala.

  32. Jamani mi nina mtoto wa miezi 10 kila akipelekwa kliniki wanasema kapungua uzito.naombeni ushauri nimpe nini aongeze kilo/uzito?

  33. Mama asante kwa ushauri wako mzuri.Mimi ni mama wa mtoto wa miezi mitano.naomba kujua ni vyakula gani naweza kumpatia kwa sasa kwani mimi ni mujariwa ninaingia kazini asubuhi mpaka saa tisa jioni.nitafurahi kupata list ya mlo wake.asante

  34. asante kwa mafundisho yako mama. naomba unisaidie kwa hili, nina mtoto wa mwaka anakula kila aina cha chakula kwa sasa ila hapendi maziwa mengine ila chai ya maziwa anakunywa. kwani siwezi kumuwekea sukari na iliki kidogo ili kumpa harufu kwenye maziwa ya ngombe. nitafurahi sana kupata majibu yako.

  35. Nashukuru sana kwa ushauri wako mzuri mshauri, mimi mtoto wangu ana miezi saba, alivyokuwa na miezi sita nijaribu kumpa cerelac alipata choo kibaya, je nijaribu tena kumpa maana umesema inaleta afya kwa mtoto.

  36. Kwa iliki kwakweli sio vizuri kumwekea mtoto mdogo viungo kwenye chakula au kinywaji lakini unaweza kumwekea kasukari kadogo au asali mbichi kwa mbali.

  37. Kila mtoto ni tofauti na mwingine, inawezekana akawa ana allergy na kitu kilichomo kwenye cerelac hivyo usimlazimishe subiri akue hadi mwaka ndio ujaribu tena. Ubarikiwe

  38. Mimi mwanangu nilianza kumsagia viazi kwenye blender akiwa na miezi 7, vinakuwa ni viazi vilivyochemshwa na supu ya samaki au nyama au na maziwa. Anavyozidi kukua unaweza kumsagia pamoja na samaki au nyama kidogo au hata njegere na mboga za majani. Kuwa mwangalifu na samaki, miiba midogo ni hatari hivyo tumia samaki wakubwa wenye minofu mikubwa na miib mikubwa unayoweza kuitoa yote.

  39. Ahsante aunt kwa kutuelimisha kuhusu watoto, kwani klinik za sasa hivi zaidi ya kumpima mtoto kilo, basi hakuna masomo ya watoto kama zamani

  40. samahani kwa kuwa nje ya topic, njia gani nzuri ya kutumia kuhusu uzazi wa mpango, mbali na calenda na condom, maana naogopa sana hizi njia zingine, naomba ushauri Mpendwa

  41. kuhusu njia nyingine hutegemea sana hali ya mtu mwenyewe na sio kila njia inamfaa kila mtu, ni vyema ukaonana na mtaalamu wa uzazi wa mpango ili uweze kupata maelezo ya kina na kujua ipi itakufaa.

  42. Nashukuru sana dada kwa somo lako zuri kuhusu lishe ya mtoto,pia ratiba uliyotupatia ni nzuri nafikiri ikifuatwa vizuri ukuaji wa mtoto unakuwa ni mzuri. Mtoto wangu ana miezi 9

  43. Mungu akubariki sana kwa kutuelimisha. Mtoto wangu ana miezi 9. Nitaifuata hiyo ratiba ya chakula. Maziwa gani ya kopo ni mazuri? Je naweza mpa ya ng’ombe? Thanx

  44. shalom!
    mimi nina mtoto wa miezi tisa hawezi kula tunda mwenyewe kama mshauri anavyotuasa ila nitamzoesha kula tunda mwenyewe kwa sasa maana nimepata akili mpya.

  45. shalom dada!
    je mtoto mchanga ni vema apewe maji? kutokana na joto la jiji letu hili wanatoka jasho sana>

  46. shalom
    Ninavyujua ni kwamba mtoto mchanga hapaswi kupewa chochote zaidi ya maziwa ya mama hadi amefikisha umri wa miezi sita..kwa afya bora na kwa usalama wa mtotto wako.

  47. habari,
    mimi nina mtoto wa mwaka 1 na mwezi 1 tangu nimejifungua mtoto wangu anapenda kula mnoo, na mbaya zaidi mimi sishindi nyumbani naenda kazini siku sita za wiki, jamani mwanangu sasa hivi kitumbo kinazidi kuwa kikubwa na kikugumu na anakula kila aina ya chakula. nimejaribu sana kumpangia dada ratiba lakini bado….. naomba ushauri wako mama.

  48. Mbarikiwe sana,

    Lakini hamjaniambia jinsi ya kutengeneza unga wa lishe kwa mtoto.

  49. Kuna aina nyingi za unga wa lishe na ni vyema ukatambua mtoto wako anapendelea nini au nini kinamdhuru ili unapotengeneza unga ujue nini uweke na nini usiweke. Nitaelezea jinsi ya kutengeneza unga wa lishe muda mfupi ujao.

  50. Mama Antony Says:
    Mtoto wangu amezaliwa na uzito mzuri 2.9kg miezi ya mwanzo alipanda vizuri
    alivyofikisha miezi minne akaanza kupanda taratibu, cha kunitisha mtoto
    hanenepi, japo najitahidi kumlisha vizuri na vyakula nilivyopangiwa na daktari
    wa watoto je atakuwa na tatizo gani naomba msaada wako.

  51. Shalom
    Kwanza ningependa kujua kama mtoto wako bado ananyonya na je maziwa yanatoka ya kutosha? Na je hicho chakula huwa unahakikisha amekula na kushiba au unamwachia msichana wa kazi? Pia afya sio lazima awe mnene sana ila tu kwenye kadi ya kliniki awe kwenye rangi ya kijani.

    Kwa sasa ana miezi mingapi na alianza chakula akiwa na umri gani?

  52. Mammy Lizzy says
    Ubarikiwe sana mumy kwa huduma nzuri sana Mungu aliyokupa .
    Me mtoto wangu ana miezi 7 wakati akiwa na miezi sita nilimuanzishia lishe yenye mchanganyiko wa karanga lakini akapata homa kali sana doctor akaniambia nisimchanganyie kitu chochote sasa anazidi kukua na bado naendelea kumpa uji huo wa dona tu ambao hauna kitu je ni sahihi au nifanyeje kwa sasa japokuwa afya yake ni nzuri tu kwani nampatia mtori pia ahsante.

  53. Samahani kuchelewa kujibu, watoto huwa wanatofautiana sana kuhusu napoleon ya vyakula hasa wanapokuwa chini ya mwaka mmoja. Sababu umeshajua nini kinamfaa endelea macho hivyo hivyo na usimchanganyie na chochote. Baadaye anavyozidi kukua kwa ushauri wa daktari utakuwa unambadilishia unga mfano wa ulezi pekee n.k Jambo la muhimu mtoto awe na afya. Uwe pia unampa supu ya mchicha, samaki (uwe mwangalifu sana na miiba) na maharage.

  54. Hi, mtoto wangu alizaliwa, akachelewa kulia, hadi sasa ana miez 9, hajaweza kukaa vzr, shingo haijakaza. Je kuna uwezekano wa mtoto huyu kukua na kuwa kama wengine?

  55. Pole sana kwa tatizo la mtoto wako, namwamini Mungu kwake hakuna lisilowezekana hata hili la mtoto wako anaweza. Ni vyema ukampeleka kwa daktari wa watoto kwa ushauri wa kitaalamu.

  56. Mungu azidi kukubariki na kazi unayoendelea kuitenda. mimi naitwa mama Clara, binti yangu ana miezi sita na wiki tatu sasa, nimemnyonyesha kwa miezi sita mfululizo na ana afya njema. kwa wiki mbilizilizopita nimekuwa nikimpatia vyakula vingine mbali na maziwa ya mama. nimeshampa uji wa mahindi, nimempondea viazi na ndizi, nataka nimjaribishie uji wa mchele, sijajua jinsi ya kuuandaa. naomba unisaidie mpendwa.

  57. Hongera kwa matunzo mazuri ya motto. Unaweza kusaga mchele na kumpikia kama uji, wengine wanaweka sukari na wengine chumvi kidogo, au pia unaweza kupika kama wali uwe rojo kisha unasaga kwenye blenda.
    Nakutakia malezi mema

  58. shalom
    mwanangu ana miezi minne,nahisi maziwa yangu hayamtoshi,je nimuanzishie vyakula gani? alipofikisha miezi 3 nlikuwa namchanganyia maziwa ya ng’ombe kidogo.ahsante.

  59. Nakushauri usimwanzishie kwanza vyakula bali uwe unampa maziwa mbadala kuongezea na maziwa yako, us ng’ombe au formula. Mara nyingi mama akirudi kazini maziwa hupungua, jirahidi kunywa maziwa kwa wingi pia.

  60. Asante sana dada kwa kutusaidia na mungu akubariki sana, mimi ninamtoto wa miezi 2 na nusu na ni mfanyakazi unaweza kunielewesha jinsi ya kukamua maziwa yangu niweze kumuachia maana narudi jion sana na napenda aendelee kuyapata

  61. Shalom,
    Kuna pump maalum za kukamulia na jinsi ya kuyahifadhi, bahati mbaya sijawahi kukamua hivyo sijui unayahifadhi vipi. Nitauliza kwa wataalamu kisha nitakujulisha.
    Ubarikiwe.

  62. shalom mtu wa mungu binti yangu ana mwaka lakin uzito wake hauongezeki tangu akiwa na miezi nane na hapendi uji wala maziwa namnyonyesha usiku tu kutokana na sababu za kikazi.nishauri nimpe nini aongeze uzito

  63. hi,samahani,mim ninamtoto wa kike ana umri wa miezi 4,nampa maziwa ya Intact Formula,ila choo chake kinakuwa cha kijivu eti ni kwa nini?na je naweza kumpa uji au chakula kingine tofauti na maziwa?maana mimi natoka job saa 9 jioni

  64. shalom
    mtoto wa mwaka mmoja anaweza kula vyakula vingine vingi kwa sababu ameshakuwa mkubwa na pia kwa sababu anamichezo mingi ni vyema akapewa chakula chenye virutubisho vyote na mara kwa mara ili aweze kuwa na afya njema. Kumnyonyesha usiku tuu haina shida ila pia mchana awe anapata maziwa mengine. Nitaweka hapa mlo wa mtoto wa mwaka hadi mwaka na miezi sita. Ubarikiwe

  65. Kuhusu choo mpeleke kwa daktari ili aweze kutambua kama choo kimesababishwa na maziwa au ana tatizo lingine. Kwa miezi minne ni vyema kumpa maziwa mchana na usiku ila pia unaweza kumwanzishia uji mwepesi mara moja kwa siku (asubuhi) ila usiwe mchanganyiko wa nafaka nakushauri uwe wa dona pekee hadi afike miezi sita.

  66. nashukuru sana kwa kupata kile kilichokuwa kinatusumbua ktk vichwa vyetu while tuna mtoto ana umri wa miezi saba kwa sasa , kabda ajatimiza miezi saba alipatiwa uji wenye mchanganyiko wa nafaka akatokwa na vitu na ukurutu mgongoni ! amepelekwa hospital akapewa dawa vikaisha kbs! lkn tunashangaa umejirudia tena na ule ugonjwa hatujui nini kinasababisha kwani kuna wkt analia kama vile tumbo linamuuma na kupata cha rangi(anahara) ahsante ubarikiwe.

  67. Shalom

    Kawaida inafaa unapiomuanzishia mtoto wa miezi sita uji usianze na unga wa nafaka mchanganyiko. Anza na mahindi ambayo hayajakobolewa na kisha unamjaribu nafaka nyingine moja moja maana tymbo lake bado halijakomaa. Pia Uwe unampa na papai kidogo na maji ya kunywa kidogo. Guo ukurutu inaweza kuwa ni allergy hivyo muone daktari wa watoto atakusaidia.

  68. Asante kwa ushauri mzuri, ni kweli wataalamu wanashauriwatoto wanyonye niezi sita then ndo waanzishiwe vyakula vingine, kama tahitaji maziwa mbadala, apewe formula na ya ng’ombe ni vizuri wapewe akifikisha mwaka.

  69. asante sana kwa huduma yako mama, ila mimi nina swali vipi kuhusu vitunguu swaumu kwa mtoto wa miezi nane na kuendelea

  70. Kuanzia miezi nane unaweza kumpa vitunguu saumu kwenye chakula chake ila kwa kiasi kidogo ila kabla ya miezi nane haishauriwi.

  71. helo,
    mimi mwanangu anamiezi 6 ndio amefikisha jana,nataka nianze kumpa chakula na matunda.naomba kuuliza je naweza kumpa tunda nusu labda parachichi/papai/tikiti maji halafu nikalikata kipande nusu then naweza kuweka frijini kipande kinachobaki halafu nikaja kukitumia tena tunda lililobaki nikampa tena mtoto baadae kipande kilichobaki?

  72. Unapoweka tunda kwenye friji kwa ajili ya mtoto ukilitoa hakikisha halina baridi kabisaa ndio umpe, unaweza ukaliweka kwenye chombo kisha ukadumbukiza kwenye maji moto ili lipate joto. Ni sawa kufanya hivyo ila lisikae siku nyingi

  73. Habari mtumishi wa bwana
    mi nina mtoto wa miezi nane ana afya nzuri na anakaa vizuri tu ila hajaanza kutambaa nini tatizo na je mtoto wakiume huanza kutambaa akiwa na umri upi na nifanye nini ili aanze kutambaa ntashukuru kwa msaada wako

  74. Sio jambo la kushangaza kwa baadhi ya watoto kuruka stage ya kutambaa na kusimama moja kwa moja na kutembea, na wengine huchelewa tu kutambaa ila baadaye watatambaa kidogo na kisha kuanza kutembea. Kama mtoto wako anakaa vizuri, anaweza kushika toy na kuchezea kwa mikono miwili akiwa amekaa usiwe na wasiwasi. Ili kumfanya atambae mkalishe chini halafu uweke vitu anavyovipenda mbali naye kisha umuache, atatafuta njia ya kuvichukua hadi atatambaa, iwe ni kwa tumbo au magoti.

  75. hi,asante kwa huduma mungu akubariki,naswali namtoto wamiezi9 hajaota meno paka leo sasa nitatizo au niukuaji tu wa mtoto yeye yuko vizuri tu ntashukuru kwaushirikiano wako

  76. habari mtumishi naomba unisaidie ninamtoto mdogo wa miezi saba anaafya nzuri na anakaa kwabahati mbaya nimejigundua nimjamzito tena sasa je naomba ushauri nifanyeje ilinisimuathiri huyu mwingine najenaweza endelea kumnyonyesha haitamdhulu

  77. Mtumishi Mungu akubariki sana kwa kutuelimisha. Je kwenye uji wa mtoto tunaweza kuweka blue band au tanbond? Asante.

  78. nimefurah sana kupata mtiririko huu wa vyakula ikiwa ndo mwanangu anatizimiza miez 6 na anaanza kula vyakula mchanganyiko.

  79. mtoto wangu ana umri wa mwaka mmoja na miezi minne, hapendi kabisa maziwa ya ng’ombe. Je nifanyeje?

  80. Shaloom.
    Mtoto wangu ana miezi saba anakataa kula na akilazimishwa anataapika. Naomba ushauri wako mpendwa.

  81. Shaloom Mama,
    naitwa Glory,ninamtoto wadada yangu ambaye alifariki akaniachia mtoto wa wiki 2. lakini sasa anaumri wa mmwaka na miezi 3.hapendi chalula chochote zaidi ya juice ya matunda mchanganyiko na mtori tu.tukimuwekea wali akijaribu punje 1 ya wali,hawezi kabisa anaweza akatapika.ila mtori tunamchanganya na nyama ama dagaa, na juice huwa ya embe,parachichi,papai na karoti ama nanasi.je nisawa?sijajua nimjaribu na chakula gani tena.kwa ufupi chakula chochote cha kufuna hawezi, anatumia vya majimaji tu,sasa nahisi hata pata uzito unaotakiwa.je nimjaribu na chakula gani tena?

  82. Shalom
    Usiwe na wasiwasi, watoto hutofautiana sana katika ukuaji, kuna wengine hupata jino la kwanza wakiwa na mwaka, kama anakuwa vizuri, afya njema usiogope.

  83. Ni vyema ukamuachisha na kumtafutia maziwa mbadala. Mkazanie kumlisha vyakula vya aina tofauti na kumpa maziwa ya formula au ng’ombe. Usiogope, watoto ni baraka toka kwa Mungu naye hutupatia kwa makusudi maalumu.

  84. Jaribu kumchemshia na kuweka majani kidogo wengine hawapendi kunywa maziwa moja kwa moja lakini ukiweka majani ya chai wanaona kama ni chai hivyo wanakunywa bila tatizo.

  85. Jaribu kumpa uji wa dona bila kuchanganya na ulezi. Mbadilishie chakula hadi ujue anapendelea nini. Pia usimoe chakula kila saa, mpe muda wa kusikia njaa na utaona mabadiliko.

  86. Nimeguswa sana na jinsi ulivyojitolea kumlea mtoto huyo. Kwake wewe ndio mama yake mzazi na kwa hakika Mungu akubariki sana kwa upendo huo.
    Kuna watoto wanashindwa kutafuna hadi wanafika miaka mitatu, sio kwamba wanatatizo bali ni ukuaji wao jinsi ulivyo. Mtori unaompa hauna shida kabisa, ila pia umpe na uji wa lishe ili apate nafaka, umsagie wali kwenye blender ukichanganya na mboga za majani au njegere au maharage. Pia umpe matunda uliyopondaponda mfano ndizi mbivu, parachichi, embe na papai.

    Mungu akubariki sana.

  87. Shalom,
    asante kwa kutuelimisha mimi ni mama mpya na mtoto wa miezi9,kwa kweli nimefurahia uashauri wako.ubarikiwe.

  88. Asante kwa hiyo elimu. mtoto wangu ana miezi 6 naweza kumpa chakula chochote bora niiponde ponde iwe laini? mimi ni mama Mary.

  89. Shaloom. Mtoto wangu ana miezi anakula vizuri lakini anapungua uzito sijajua ni kwanini, naimba ushauri wako. (ana miezi 11)

  90. Akhsante mama Kenneth kwa somo na wadau wote wanaouliza maswali na kutushirikisha uzoefu kuhusiana na watoto!
    Mimi mtoto wangu ana miezi tano na nusu nampa maziwa yangu na mbadala nikiwa kazini. Maziwa mbadala anasumbua sana mara nyingi anakataa. Ameanza kukaa mwenyewe na shingo yake imekakamaa- namshukuru Mungu. Tatizo ni kunywa maziwa, hapendi!
    Jamani huyu binti yangu toka atimize miezi 5 anatafuna sana. Akiwa yupo tu katulia anaanza kutafuna, utamwanagalia mdomoni kama kuna kitu lakini hamana.na akiona mtu anakula atamwangalia hadi huruma then nae anatafuna kwelikweli! Lakini chakula chake (maziwa mbadala) hapendi. Je, nimechelewa kumwanzishia chakula? Tulipenda uji na vitu vingine aanze akiwa na miezi 6.

    Nawashukuru wote na mmebarikiwa!!

  91. Umenikumbusha mtoto wangu ambaye anamiezi kumi sasa alipokuwa na miezi minne alikuwa anakiangalia kijiko tangu unapochota chakula hadi unafikisha mdomoni huku akitamani naye apewe. Hiyo ni ishara mojawapo kuwa yupo tayari kuanza kula. Kutafuna inawezekana fizi zinawasha kuashiria meno kutoka au pia anaigiliza mnavyokula hivyo yupo tayari kuanza kula.

    Kukataa maziwa mbadala inawezekana ikawa hapendelei aina ya maziwa mnayompa, mara nyingine watoto huchagua sana, mimi nilibadili maziwa mara 3 kupata maziwa anayoyapenda na sasa anakunywa bila shida yoyote.

    Sio vibaya kumuanzishia mtoto chakula chepesi akiwa na miezi 5 na ameshakaa na kuonyesha dalili za kutaka kula, unaweza anza na uji wa nafaka moja uliosagwa mara mbili na mwepesi kabisa. Akiendelea kuchukia maziwa hakikisha chakula chake kinapikwa kwa maziwa tu ili aweze kupata virutubisho anavyohitaji.

    Hongera za malezi

    Swal

  92. asante kwa kutuelimisha mtu wa Mungu,ila naomba unisaidie kitu kimoja,mwanangu anapenda sana kulala yani mpaka ratiba ya kula inavurugika sasa naomba unishauri tu je, niwe namuacha mpaka hapo atakapo amka mwenyewe au muda wa kula ukifika kama bado amelala niwe namuamsha?tafadhali naomba unieleweshe katika hilo.

  93. Mama Keneth akhsante kwa ufafanuzi na ushauri; UMEBARIKIWA. Nimemwanzishia vyakula vyepesi sana lakini bado naona hafurahii chakula. bado najitahidi kupata chakula atakachopenda na Mungu anisaidie mana mara nyingine inakua ngumu kweli kumlisha. sasa ana miezi 6 na nusu.
    Kwa mara nyingine nawashukuru wote kwa ushauri na kutushirikisha uzoefu. mmebarikiwa.

  94. shalom
    Mtoto wako hujaniambia ana umri gani. Mimi mtoto wangu alipokuwa na chini ya miezi sita alikuwa anapenda sana kulala hivyo nilikuwa namnyonyesha akiwa usingizini na alikuwa ananyonya vizuri tu, ila kwa sasa ana miezi kumi kama muda wa kula umefika namuamsha taratibu kisha namchangamsha kwa kutembea naye na kuchezacheza naye ili aweze kula maana ratiba ni lazima ifuatwe kwa afya bora. Ni vyema kumuamsha ili ale kwa muda ule uliopangwa la sisvyo hatamaliza share ya siku hiyo na kila siku ratiba itakuwa inavurugika.

  95. asante sana kwa kunielewesha,mwanangua ana miezi 8 sasa,nitakuwa namuamsha

  96. Amani ya Bwana iwe nanyi!!!!!!!!!!!
    nina mtoto wa miezi miwili, baada ya mwezi nitaanza kazi na nikianza kazi huwa nachelewa sana kurudi,
    je ninaweza kumuanzishia mtoto wangu maziwa ya ng’ombe au formulas kila siku mume wangu ukimueleza kuhusu hilo anakataa katakata kumpa maziwa ya aina yeyote mpaka afikie miezi sita je ataweza kujua kunyonya maziwa mengine baada ya muda huo?

  97. Asante kwa kutuelimisha mtumishi, mimi nina mtoto wa miezi nane ila tangu nimeanza kazi full time amegoma kunyonya anakataa kabisa japo alinyonya vizuri mpaka naanza kazi imebidi nimpe maziwa ya kopo ila sina amani kabisa naomba ushauri,

  98. Ubarikiwe sana mpendwa kwa mafundisho mazuri, yamenisaidia sana na nitayatumia kwa mtoto wangu mwenye umri wa miezi sita na wiki mbili, be blessed

  99. Pole sana mama Collins, najua jinsi gani jambo hilo linaumiza. Mimi mtoto wangu wa kwanza alikataa kunyonya akiwa na miezi sita baada ya kurudi kazini nilihangaika sana ila hakukubali kabisa.

    Wa pili yeye nilijua atanyonya sana maana nilikuwa siendi kazini lakini naye pia alipofika miezi saba kwenda nane akakataa kunyonya. Sifahamu sababu inayomfanya mtoto akatae kunyonya ila huna budi kumpa maziwa mbadala na lishe nzuri. Usivunjike moyo hauko peke yako, hizo zote ni changamoto za malezi. Ubarikiwe

  100. Hongera kwa kupata mtoto. Kama ofisini kwako watakuwa wanakupa ruhusa masaa mawili kabla ya muda ili ukanyonyeshe unaweza kununua pump ukakamua maziwa yako ukahifadhi vizuri akanywa mara mbili ukiwa haupo then jioni unarudi na kumnyonyesha. La sivyo huna budi kumwanzishia formula milk, hilo halina mjadala maana mtoto lazima ale. Kwani mume wako yeye anavyokataa anatoa alternative ipi? Au ikiwezekana chukua likizo isiyo na malipo kwa miezi sita, a little sacrifice for your baby is worth.

  101. Thnks a lot kwa kutupa somo zuri,binafsi nimelfurahia sana coz ndio nimeanza malez ya mtoto,be blessed!

  102. Nashukuru nimefunguka kwa mengi baada ya kusoma haya maelekezo mazuri,anayotoa Mama.Mwanangu anatarajia kufikisha mwezi miinne na nilikuwa na wazo la kumwanzishia chakuna yani uji,ingawa mama yake anamaziwa ya kutosha sana,sas hilo wazo linaondoka anyonye mpaka mezi sita.
    Pia naomba kuuliza kwani mie nimemwandalia uji wa mwohogo je nimzuri kwa mtoto anaanzakula?

  103. womanofchrist.Je uji wa muhogo unafaa kuchanganya kwa mtama mweupe.ndio lishe yangu ya kwanza nataka nianze kumtengenezea mtoto.Naomba ushauri.Na mtoto kiwa chini ya mezi sita anaweza kupewa chungwa likachanganywa na maji kidogo?

  104. tunashukuru kwa ushauri wako mzuri mimi ni miongoni mwa akinamama wanafatilia lishe ya mtoto lakini mtoto wangu hapendi kula kabisa hadi nashindwa cha kufanya na sasa ana mwaka mmoja. naomba ushauri mimi mama Ryan

  105. nimefurahi sana kwa somo lako la kuelimisha mungu akubariki,nina mtoto anakaribia miezi 6 je? ina luhucwa kumpa juice?

  106. Hi,mm ni mama mpya mwanangu ana miezi 3 na nusu ana afya nzuri tu ila anapenda sana kulambalamba vitu hasa nguo,na kung’ata,pia ananing’ata sana.je inakuwa nn?

  107. nimependaelimu yako hasa kwa watu ambao wanakua bado hawana familia ni wakati wao wa kujipanga na kuhakikisha wanapobahatika kuwa na watoto wanayafanya hayo yote kwa umakini zaidi ili kuwa na familia iliyo boara zaidi.

  108. nashukuru sana kwa kupata kile kilichokuwa kinatusumbua ktk vichwa vyetu while nina mtoto ana umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja kwa sasa , kabda ajatimiza miezi saba alipatiwa uji wenye mchanganyiko wa nafaka akatokwa na vitu na ukurutu mgongoni ! amepelekwa hospital akapewa dawa vikaisha kbs! lkn tunashangaa umejirudia tena na ule ugonjwa hatujui nini kinasababisha,naomba msaada wa dk wa watoto mzuri wa allegy maana nahisi ni allegy.
    pia naomba ratiba ya chakula cha mtoto kuanzia mwkaa mmoja hadi miaka miwili dada,ulituahidi utatutumia,

  109. Nashukuru kwa kupata kile nilichokuwa nataka.Mungu awabariki sana.ila mimi nilikuwa nashauri wamama amabao watoto wao wanakoa wapendelee kuwapa watoto wao mafuta ya samaki kila siku hata kama hakooi wewe mpee tu ni mazuri mno,au asali mpe kila siku kama anakoa au hakohoi ni nzuri sana.Kuhusu uji wa mtoto pendelea kuwa na lishe sio mchanganyiko uwa watoto wanakinai anaraka sana.kuwa na unga wako wa dona pekee,unga wa mchelee pekee,mtama pekee,ulezi pekee,leo mpikie dona,kesho mtama,siku inayofuta mchele,utaona mabadiliko sana.Mara nyingi uji mchanganyiko wa karanga sio mzuri unawapa watoto allerge sana na Dagaa.Asanteni.

  110. tatizo hili linawapata wamama mwengi, sijajua sababu maana wangu naye alikuwa hivyo na alipofika miezi saba alikataa kabisa. Jaribu kutompa kitu cha kula mchana nadi asikie njaa kabisa kisha ndipo umnyonyeshe nadhani anaweza kunyonya sababu ya njaa.

  111. sijawahi kusikia kumpa mtoto uji wa muhogo, naomba ujaribu kuongea na daktari wa watoto kuhusu unga wa muhogo wa watoto.

  112. Mtoto chini ya miezi sita asipewe chungwa kabisa maana ni tunda lenye asidi.

  113. Pole sana mama Ryani
    Tatizo lako sio kwako peke yako, jaribu kumbadilishia chakula hasa kama unampa uji wa lishe, mpe dona, kisha ulezi, mtama kila kimoja peke yake. Vile vile mpe matunda kwa wingi hasa nyanya na mengine yanaongeza hamu ya kula na pia kumuongezea vitamini. Mpe papai, parachichi, maembe, tikitimaji, ndizi n.k

  114. Si vyema kumpa juice, ila unaweza msagia matunda na kumpa mfano papai, parachichi, embe bila kuweka maji, unasaga unampa kama uji.

  115. Watoto wana namna nyingi za kuyafa hamu mazingira yao, atakuwa anajaribu kupata test ya vitu tofauti. Wengine huwa wanapata dalili za meno mapema hivyo huwa wanakuna fizi zao kwa kung’ata vitu mbalimbali.

  116. Inawwezekana ana allegy na kitu k imojawapo unachoweka kny uji, maranyingi watoto hupata allergy ya karanga na dagaa, au pia kama unaweka blueband. Jaribu kuviondoa hivyo vitu ukiona bado hali inajirudia mrudishe tena kwa daktari wa watoto.

  117. Habari!mwanangu Ana umri wa mwaka mmoja na miezi Saba..tatizo ambalo linasumbua ni la kukataa kula chakula anachopewa zaidi anapenda sana Kunywa Maji ya Kunywa na juice na maziwa ya mama..tumejaribu kila njia lakini hakuna mafanikio..tunaomba ushauri wako..Ahsante

  118. Mpatie mtoto wako juice ya ubuyu mara kwa mara kwani inaleta hamu kubwa ya kula. Mama Alicia

  119. Mama Ethan George , Asante sana kwa ushauri na ninapenda sana somo hili linanielimisha sana kwani nina mtoto wa miezi sita na sikuwahi kuelewa natakiwa kumpa lishe gani na kwa ratiba gani?

  120. Glory!! Mungu akuweze ktk huduma hii ya kuelimisha wazazi kwa ajili ya lishe kwa wtt ambao ni taifa la kesho! sina swali kwani mengi umeshaulizwa na kuyajibu vzr nitayafatilia. Ubarikiwe sn.

  121. nafurahi sna ninaposoma maelezo ya malezi, nina watoto wawili wa miaka mitatu na wa miezi mitatu. huyu wa miaka mitatu hapendi kabisa kula, sa cjui anakinai vyakula fulani. plz mama keneth naomba unisaidie ushauri juu ya huyu binti yangu wa miaka mitatu vyakula vya kula ambavyo mtoto anapendelea kula. asante sana

    ubarikiwe.

  122. Shaloom! jamani nimebarikiwa sana na mada. Mimi mtoto wangu ana miezi kumi sijawahi kublend chakula chake, sasa anakula vyakula mchanganyiko na unga wake wa uji namchanganyia mahindi, mtama, uwele, karanga na mchele haujamdhuru, ila tatizo ni moja mbona hawezi kumeza kitu akiwa anameza anakuwa kama anakabwa ni koo lake halijazoea? nisaidieni nijue nifanyaje ili ata nkimpa tunda aweze kung’ata na kutafuna mwenyewe. pia je amechelewa kujifunza kutafuna? naomba ushauri ndugu zangu. Ubarikiwe

  123. shalom wapendwa katika bwana.
    mimi nina tatizo, mwananguana mwaka mmoja na miez 3, hapendi uji wala chakula chochote nnacho msagia…anapenda kula vitu ninavyokula 2 kama ugali,wali,nyama ya kurost,maharage,chipsi na vingine, naombeni ushauri ni vyakula gani niwe namtayarishia katika umri wake.

  124. shalom
    je naweza kutengeneza chakula na kusaga na kukitunza kwa muda kama wa wiki hivi? kwa kukiweka kwenye freezer? ukiacha matunda. na je kiini cha yai ni kile kilichochemshwa au kiwekwe kibichi kwenye uji? women of christ you really touched me, ahsante sana.
    ETM

  125. Watoto wengi wa miaka mitatu husumbua sana Kula. Karibu kumbadilishia vitu ambavyo hamna mazoea ya kuvipika, mfano viazi mviringo unakata nusu na kukaanga anakula na mboga za majani au mchuzi wa nyama, tambi na makaroni, pilau maana watoto wengi wanapenda pilau na wali wa maharage. Pia mtengenezee juis kwa wingi na matunda. Mpe chakula kidogo kidogo na tofauti tofauti mara kwa mara mfano asubuhi akiamka uji, saa nne chai na mkate/maandazi/chochote unachoona anakipenda, mchana ugali/viazi/n.k jioni maziwa/ juis na yai la kuchemsha, kiazi cha kuchemsha n.k na usiku tena chakula kidogo. Usimshindilie chakula kingi kwa wakati mmoja.

  126. Miezi kumi bado mdogo kuweza kumeza vitu maana bado hajaweza kutafuna vizuri, nenda naye kidogo kidogo wala usiwe na hofu muda ukifika atatafuna na kumeza bila wasiwasi kwa sasa mpondee pondee kwa kijiko hayo matunda kisha ndio umpe.

  127. Wala usiwe na wasiwasi kwa mwanao kupenda vyakula mnavyokula mpe tu avizoee lakini sababu hali hadi akashiba uji ni muhimu sana kwake. Angalia post ya lishe ya mtoto miezi 12-18 utaona vyakula vingi unavyoweza kumpa.

  128. Yes unaweza kutengeneza na kuweka kwenye plastic containers kila conteiner moja unaweka mlo wa mara moja, ukitoa unadefreez na kumpa. Usiweke kingi mahali pamoja na kudefreeze ukatoa kidogo kisha ukarudisha, hapo kitaharibika.

    Yai ni bichi kiini chake unakoroga na unga hadi kilainike kisha unapika. Kutenganisha kiini na ute toboa yai tundu dogo kisha mwaga ute wote utabaki na kiini.

  129. Nashukuru kwa mafunzo unayotupatia. mimi mtoto wangu ana mwaka mmoja, je, naweza kumpa juice za aina gani? ubarikiwe,

  130. Mimi dada nashukuru sana kwa ushauri wako mzuri kwa jamii, ila mimi nina mtoto wa miezi mitano na nusu ila nianza kumpa uji akiwa na miezi 4 na wiki moja, na nilimwanzishia lishe mchanganyiko moja kwa moja, ila anakula vizuri tu, na maziwa ya ngombe ndo nampa kwa weak lita tano je ni sahihi kumpa lita tano kwa wiki???

  131. Nisawa maana mtoto wa miezi mitano hatakiwi kula chakula kigumu zaidi ya mara mbili kwa siku hivyo mlo mkuu ni maziwa.

  132. Juice ya kutengeneza mwenyewe ya maembe, mchanganyiko wa maembe passion na tikiti maji, tikiti maji lenyewe, machungwa, maembe na parachichi n.k

  133. Nashukuru sana kwa ushauri wako mzuri kwa jamii;mimi nina mtoto wa miezi mitano amekataa kabisa maziwa ya kopo na mimi ni mfanyakazi natoka saa tisa kazini je nimpe nini cha kumfaa mpaka nitakaporudi;tangu alipokataa ni wiki sasa nimekuwa nikimpa uji mwepesi saa nne basi mpaka ninaporudi ndiyo ananyonya naomba ushauri.

  134. Mtafutie maziwa ya ng’ombe na umchanganyie na maji, asubuhi hadi saa tisa ni muda mrefu sana kwa mtoto wa miezi mitano kukaa bila maziwa

  135. Shalom watu wa Mungu. Naomba kuuliza ni Cerelac gani nzuri kwa mtoto wa miezi tisa? Na kutoka wapi?

    Asante

  136. mama sifuel,ahsante sana mama kutuelimisha.nimejua lishe bora kwa mtoto.mimi na watoto wawili mapacha wa kiume na wakike wa miezi saba.nawapa chakula sawa uji wa lishe,mtori maziwa ya ng’ombe na na supu ya maharage na mboga za majani na tunda embe au papai.lakini tatizo moja mtoto mmoja mtoto wa kike anaongezeka taratibu kiasi kwamba yule wa wakiume anakilo 9.7 wakati wa kike ana kilo 7.8,nimewjaribu kumuona daktari akanishauri ni hari ya kawaida,lakini nesi kasema niongeze kipimo cha chakula nimejaribu kuongeza mwanangu wa kike anakula hadi anataka kutapika na hawezi kumaliza naona namuonea.mamamkwe wangu kanishauri kumpa kiini cha yai lisilochemshwa je halina madhara.naomba ushauri mamaangu maana ndo wanangu wa kwanza.

  137. Hongera kwa baraka ya watoto. Ni kweli mara nyingi hutokea pacha mmoja akakua kuliko mwingine, usimzidishie kipimo mpe tu sawa na umri wake. Kiini cha yai hakina tatizo unaweza pia pikia kwenye uji ila asile zaidi ya mara tatu kwa wiki.

  138. Asante kwa ushauri mama yetu, Naitwa mama sam ubarikiwe sana, mie nina swali moja mama kwa sasa dsm yetu ina joto sana, na tunashauriwa tusitumie feni kwa watoto wetu, je vipi kuhusu AC- kwa kuweka ubaridi wa kawaida unaweza itumia na isimuathiri mtoto?

  139. Naitwa mama Derick, asanteni sana kwa ushauri na ratiba yenu nzuri ya namna ya kutayarisha na kumlisha mtoto, nimeipenda na kuifurahia kwa sababu na mimi nina mtoto wa mwaka mmoja na mwezi mmoja. lakini nina tatizo moja naombeni ushauri wenu kutokana na uzoefu mlionao, mtoto wangu siyo mlaji kwa kweli (yaani kwa kifupi derick hapendi kula) yaani ikifika saa ya kumlisha kwa kweli nina hangaika naye sana na hata akila ni vijiko vitatu au vinne basi anaanza kukataa na ukimlazimisha basi hata kile alichokula kidogo atakitapika. nambadilishia mlo kila siku lakini bado sijaelewa tatizo liko wapi.

  140. Asante kwa kazi yako nzuri na njema mtumishi wa Mungu mimi ni mama mwenye mtoto wa miezi sita na nusu nimejaribu maziwa yote hataki ijapokua haya ya formula anakunywa kwa sida sana hata ml 60 hamalizi je naweza kuchanganya hayo maziwa na chakula cha mtoto kwa mfano kwenye viazi?pili nauliza mtoto wangu ana uzito wa kilo 10 na nusu je kwa umri huu ni sawa?

  141. Miezi sita kilo kumi ni zaidi ya unavyotakiwa, mwanao anauzito sana mpunguzie vyakula na kumpa maziwa zaidi. Inaelekea unapompa maziwa anakuwa ameshashiba tayari. Mpe maziwa akiwa hajala kitu kwa masaa mawili hadi mawili na nusu. Mtoto wa miezi sita anahitaji analau mls 240 kwa siku na sio chini ya hapo. Maziwa ya ngo’ombe unaweza yapikia kny uji na mtori.

  142. Habari wamama wenzangu, mimi ninatatizo hili nimejifungua mtoto ana miezi 6 sasa lakini sijapata bleed sijui ni kwanini na sina ujauzito mwingine ni kawaida au nina tatizo

  143. Shalom mtumishi, ahsante sana kwa kutuelimisha nimependa mno somo lako, mi naomba ushauri mwanangu ana miezi nane ila tangu afikishe miezi sita hajaongezeka uzito amebaki na kilo zake saba tuu na hapendi kula anakula kidogo tuu ukimlazimisha akimaliza kikombe kidogo anatapika je nifanyeje?

  144. mtoto wangu ana miezi 8 hapendi kabisa maziwa zaid yakwenye kifua changu je unashauri nimpe maziwa gan mana kwa sasa nimeanza kazi,napia kuna rashez zimemtoka kama kaaleg flan sasa cjui tatizo litakua nn..

  145. Wazazi wengi hukumbana na tatizo kama lako. Usimpe chakula kingi mara moja, mpe kidogo mara kwa mara na mbadilishie kidogo kidogo. Mpe pia matunda kama papai na parachichi, bila kusahau maziwa kwa wingi maana ndio lishe yake kuu. Mpe pia supu ya maharage yasiyoungwa, supu ya mchicha (usage kny brenda uwe laini kabisa), na supu ya nyama. Uji uwe wa lishe, umsagie na karanga umwekee kenye uji, na pia yai la kienyeji (kiini pekee) mara mbili kwa wiki.

  146. Miili hutofautiana, wengine huwa hawapati hadi mwaka ila ni vyema ukionana na daktari kwa ushauri zaidi. hongera kwa mtoto

  147. shalom mtumishi. Nipenda sana blog yako nilipata ratiba ya chakula hapahapa ikanisaidia kuwalea mapacha wangu japo wao wameacha kunyonya muda huu wana mwaka na miezi sita. Je naweeza kupata ratiba ya chakula kwa umri huu? Kazi njema

  148. watotot wengine wanasumbua wakiwa wadogo wanakua na njaa saana mama zao maziwa hayatoshi wakiwa chini ya miezi 4,, sasa inabidi kuwaanzisha muji mapema hapo napo unasemaje

  149. Shalom, kuna lishe kwa miezi 12 hadi 18, angalia kwenye link ya malezi ya watoto utaiona. Ubarikiwe

  150. hi! Mm naitwa zena nina mtoto wa miezi mitano mtoto wangu anapunguwa kilo nifanyeje ili angezeke

  151. poleni na kazi ya kutuelimisha wapendwa,mwanangu anna miazi 6 na nusu sasa ila hapendi kunywa maziwa kwakuwa nampa ya Ng’ombe yapo uji unakunywa kidogo,je naruhusiwa kumpa maji ya machungwa?
    Mama Gift

  152. Naitwa Grace, mtoto wangu ana miezi 6 sasa ana kilo 9.5 anatumia maziwa yangu na ya ngombe ninapokuwa kazini, nataka aanze kula mchanganyiko kama ulivyotoa maelezo na ratiba hapo juu je inawezekana kutokana na kilo zake

  153. Naitwa Asia,tatizo langu mtoto wangu anamiezi 7 alikuwa anaendelea vzur,lakin gafla ameaza kukataa chakula kwa kwel nakosa raha ila maziwa ananyonya vzur,embu nishaur dada nifanyaje.

  154. mie nina watoto mapacha wana umri wa miezi 11 na wana kilo kulwa ana kilo nane na doto ana saba na nasu na nilijifungua kabla yaani ni njiti je kilo zao na umri wao je ni sawa naomba ushauri na hawapendi kula kitu chochote zaidi ya uji wa lishe na juice ya chungwa.

  155. Maji ya machungwa sio mazuri sana kwa watoto wa chini ya mwaka, mtengenezee puree ya matunda bila kuchanganya kama papai, embe, parachichi na juice ya matikiti maji

  156. Inawezekana, ila kwa kiasi kidogo na mara mbili kwa siku. Unapunguza maziwa unayompa na kuanza jumps chakula maana ni muhimu sana kwa ajili ya ukuaji wake, maziwa pekee hayatoshi.

  157. hi! mie nina mtoto wa miezi mitano na nusu alizaliwa njiti na ana uzito mdogo yaan kilo 5 kwa sasa nampa uji na maziwa tu. je? naruhusiwa kumpa lishe nyingine? na maziwa yangu vile vile hayamtoshi.

  158. nashukuru mama keneth kwa somo lako zuri! mimi ni mama mwenye mtoto wa miezi sita sasa nataka nijue je nikitumia maziwa ya ng’ombe mimi mwenyewe itaweza dhuru maziwa ya mtoto?

  159. Shalom.. Mwanangu ana miezi minne na wiki 3 nampa maziwa ya formula SMA Gold je na weza kumpa na maziwa ya ng’ombe pia? Mama G.

  160. Tatizo hilo linawapata watoto wengi. Mbadilishie chakula usimpe hicho hicho kila wakati na umpe kidogo kidogo kila baada ya masaa matatu bila kusahau juis ya kutengeneza, supu mbali mbali na matunda ya kupondaponda.

  161. Hapana, wewe tumia bila shida ila mtoto usimpe maana siku hizi kuna magonjwa mengi watoto wanapata kutokana na maziwa ya ng’ombe subiri hadi afike mwaka mmoja

  162. Hapana, siku hizi watoto wengi wanapata magonjwa mbalimbali kutokana na kupewa maziwa ya ng’ombe. Endelea kumpa SMA ni maziwa mazuri.

  163. Habari dada Mimi Nina Mtoto wa miezi 7 but nahofia kufanya tendo la ndoa na mume wangu kwa kuhofia kumuharibu Mtoto hivi ni kweli au fikra zangu naomba Ushauri dada.

  164. Hauwezi kumdhuru mtoto kwa kusex wakati ananyonya. Hizo ni myth zinazosumbua wengi. Wazee wazamani walitumia hivyo ili kuzuia mama kupata mimba wakati mtoto bado mdogo maana hakukuwa na utaalamu wa njia mbalimbali za kuzuia mimba.

  165. Mama Abigail,Asante kwa ushauri mamy,Abigail wangu anatimiza miezi 6 kesho,nilikuwa nawaza sana jinsi ya kumlikiza,nimepata pa kuanzia.Asante sana.MUNGU azidi kukubariki

  166. Nimekua nikijaribu kufanya kama ulivyoelekeza lakini mwanangu hatak chakula chochote zaidi ya maji na matunda. Naomba ushauri wako

  167. habari dada nina mtoto wa miezi 9 sasa kila chakula ninachompa hataki yaan vyakula kama vile mtori, uji, uji wa mchele na hata maziwa hataki je? nijaribu tena chakula gani ambacho anaweza kula? na je uzito wa kilo 7.5 ni sawa na umri wake?

  168. Mpe ugali laini na mchuzi wa maharage, kisamvu au mchuzi wa Nyama. Pia mpe wali bokoboko na mchuzi. Mpe matunda kwa wingi bila kusahau juice za matunda.

  169. Habari dada,mtoto wangu ana miezi 15 sasa je naweza tumia ratiba ipi kwaajili ya chakula chake kwa siku nzima na varieties ya vyakula.

  170. Habari dada, naitwa Mama Hasnah, mtoto wangu ana umri wa miezi kumi sasa, nilikuwa nampatia chakula mara tatu tu kwa siku maana sikuwa najua ratiba nzuri ya chakula kwake, na ana kilo 9 na nusu, naomba unishauri, kwa sasa nimkazanie kumpa aina gani ya chakula na matunda?

  171. Mpe mara tano kwa siku. Asubuhi maziwa saa tatu uji wa lishe saa sita uji tena, saa kumi matunda na maziwa, au supu na saa moja mtori. Usiku anyonye

  172. napenda kujua zaidi kuhusu lishe ya mtoto kuanzia miezi 6 na kuendelea niwe napata mambo mapya kwa kunitumia kwa e-mail hapo juu

  173. aslam alykum natumai niwazima wote mm ni mgen ktk hii blog nimesoma nanimepeda sana nimefurah sana kujifunza mambo mengi mm ndo kwanza na mtt moja n she z da first born nimesoma kuhusu mambo ya chakula kwa mtt nikaopenda sana nashukuru nimejifunza mengi ktk blog hii kuhusu lishe ya mtt

  174. nimeelimika sana Mungu awabariki, mtoto wangu aana miezi sita nafikiria sana katika kumchanganyia uji je nichanganye nafaka zipi?

  175. Anza na mahindi, ulezi na mtama. Usiweke soya wala karanga. Saga karanga pekeyake kisha unamwekea kijiko kimoja ukiwa unakoroga unga na kupika uji. Hii itasaifia kujua kama ana allergy na karanga maana watoto wengi kabla ya mwaka mmoja huwa na allergy nazo. Anza bila karanga kwa wiki moja kisha weka karanga kwa wiki moja.

  176. mtoto wwangu ana miezi 9 ila hana jino hata moja uzito wake ni mzuri yuko juu ya green anacheza vizuri anacheza bila shida
    mama Baraka

  177. habari dada, mi nina mtoto wa miezi kumi na moja sasa ila uzito wake hauniridhishi kabisaa kiasi kwamba naogopa hata kumpeleka klinik ninampa kila aina ya chakula lakini wapi! naomba ushauri wako dada hata mwili wake bado unaonekana mdogo. nifanyeje?

  178. hongera dada kwa kazi nzuri ya kuelimisha kina mama. je, kuna madhara yoyote kumnyonyesha mtoto mama akiwa mjamzito? na kama kuna madhara nini kifanyike ikiwa alinyonya kabla mama hajatambua ana ujauzito?

  179. Habari, mimi nina mtoto wa miez 10 bado hajaanza kutambaa anauzito wa kg 13 nimemnunulia baby wolker badala ya kwenda mbele na babya wolker amekuwa anarudi nyuma. naomba ushauri wako

  180. kuna doctor mmoja anafanya kazi bagamoyo hospital yy ni specilist wa watoto kama utapata nafasi nenda kamuone anaitwa doctor ali

  181. nina mtoto wa miezi sita yeye anasumbuliwa sana na mafua nafikiri ni uji niliomuanzisha utakuwa hamfai ahsante kwa michango yenu nimeipenda sana kwa kutuelimisha kwani wa mama wengi hatuna ujuzi na malezi ya kuwalea watoto tuelimisheni mukipaa coment zetu

  182. Inaonyesha mtoto wako ni mzito kuliko umri wake na hivyo anashindwa kuuhimili uzito wake na kuinua mguu. Hata akikaa kny baby walker hawezi kuiendesha hivyo inampeleka nyuma. Mpunguzie wanga na mpe zaidi protini, mboga na matunda na pia usimpe mafuta ya siagi wala karanga. Uzito huo ni wa mtoto wa mwaka na nusu. Uzito ukizidi anaweza kupata magonjwa ya moyo.

  183. asanteni sna kwa kutuelimisha sisi kina mama,mimi mtoto wangu anamiezi saba sasa na nilimuazishia uji wenye(mahindi,mchele,ngano,uwele,mtama,soya na ulezi)ila baada ya mda kidogo alianza shida ya kupata choo kigumu,nikaacha kumpa uleziktk huo mchanganyiko atleast sasa,je huo mchanganyiko ni sawa kwa lishe bora ya mtoto.

  184. hongera kwa kazi ya kutuelimisha hasa kwa tunaoanza kulea kwa mara ya kwanza.. nina mtoto wa kiume wa miezi 6, je ni sahihi kumchanganyia minofu ya samaki kwenye mtori mwanangu? na je naweza pia kuanza kumpatia supu ya maharage na njegere au
    choroko?

  185. Tumsifu yesu kritu Mamy,
    Mimi nina mtoto ana umri wa mwaka mmoja , ila hapendi kunywa uji wa lishe mchanganyiko. kila ninapo mpa anataka kutapika, nimfanyeje ili aweze kula vizuri?

  186. Yaani ubarikiwe sana Mpz, nimejifunza na naamini yatanisaidia katika kumkuza akiwa na suha njema mtoto wangu wa miezi 9.

  187. salam,
    mimi ni mama wa mtoto wa miezi minne wa kiume, kwa sasa bado nampa maziwa yangu tu bila chochote, na ana uzito wa kg7.5 je sahihi kwa umri na uzito alio nao? naweza kumpa maziwa ya formula?

  188. na ameloose gram 100 this time kwani alikuwa na 7.7kg sasa ana 7.6kg je kuna tatizo labda kwa uzito alio nao ukilinganisha na umri wa miezi minne kwa mtoto wa kiume. pia anapenda sana kula mikono yake je ni tatizo pia? asante mama kwa ushauri

  189. Daktari ninashukuru sana kwa kunipa elimu ambayo sikuwa naijuwa ya lishe ya mtoto

  190. Nimefurahi sana ulivyotuelimisha maana nina mtotow wa miezi mitano ubarikiwe sana mpendwa
    mama NASIL

  191. mmh,yan nmefurah sana kwa jins mlivyoelekeza vzur ktk hii mada kwasababu nna mtoto wa miezi tisa,asanteni na mzd kutuelimisha,

  192. Daa nashukuru kwa elimu nzur ya afya jwa mtoto,nami nitajiandb jwa huduma kama hyo pindi mkewangu atakapojifungua miezi michache ijayo…thanx come up once again.

  193. mama collins says:
    Asante kwa kutuelimisha mpendwa wetu mimi nina mtoto wa mwaka mmoja na miezi miwili hapendi kula kabisanimpeleka hosp karibu mara kazaa kwa specialist wa watoto wananipa dawa za vitamini tu na bado uzito wake huko chini sana 8.8 sina furaha kabisa pia bado hajaanza kutembea anasimamia vitu tu naomba ushauri wako lishe ulizoandika zote ndio chakula chake.nahisi kuchanganyikiwa.

  194. Mtoto wangu ana umri wwa miezi 7, lakini amepatwa na tatizo la kutokukojoa…anakojoa mara moja tu baada ya saa 24 kupita..

    Naomba ushauri…ni wa kike,halii, yupo normal ingawa tunampa vyaka vya majimaji,uji,ananyonya n.k

  195. shalom, nina mtoto wa mwaka na miez minne ni chepesi sana nimekua nikifata ushaur wako juu ya lishe yake lakini wapi. Nini inaweza ikawa ni tatizo?*ana kilo 11 sasa hivi*

  196. Nimewapenda endeleeni kutufundisha malezi bora pamoja na lishe bora safisanaaaaa

  197. Mtoto wangu hataki chakula chake kabisa kama uji, mtori. Pia hapati usingizi wa kutosha

  198. nimefurahi sana kupata.lishe ya mtoto. ninamtoto anamiezi 5 ninajianda kuanza kumpa chakula akifika miezi6.

  199. ahsante kwaelimu me nina mtoto wa miezi miwili na pia ni mwanafunzi wa chuo na nina mitihani. sielewi mwanangu atakula nn. naomba ushauri nitakapokuwa chuo

  200. Nimependa namna wed yenu inavyoweza toa elimu ya malezi ya mtoto. Nahitaji fahamu muda gani unatosha kumnyonyesha mtoto?

  201. Be blessed ndugu yangu,me na mtoto ndo anaanza mwez wa nane,anasumbua kula kweli,ila anapenda juice ya chungwa sana,na umesema c nzuri sana kwa mtoto chini ya umri wa mwaka mmoja,inamadhara gan? maana ndo nampa sana ,na pia maziwa ngombe yanamadhara kwa mtoto chini ya mwaka mmoja? maana kwa sasa anatumia maziwa ya sma.na uji wake ni dona naweka sukari na chumvi kdogo tu,vyakula vingine ni kama maini ya ngombe nasaga,njegere nachanganya na viazi karot hoho ,boga pia nachanganganya, na njegere ,hoho,karoti,,na mtori.shida aongezeki uzito vzuri, naomba ushauri wako dada.

  202. mama samuel
    Ninamtoto wa miezi mitatu na ni mfanyakazi itabidi nimpatie nini ninapokuwa kazini?
    Be blessed

  203. Mtoto wa chini ya miezi sita anatakiwa kupewa maziwa ya mama tu unapoenda kazini kamua na kumuachia ukishindwa mtafutie formula milk. Usimpe chakula hadi amefika miezi sita

  204. Pole na majukumu mtumiaji wa Mungu, nina mtoto wa miezi Sita na nusu alivyofikisha miezi mitano nilimwanzishia uji wa dona na Katanga baada ya wiki mbili nikamwanzishia lishe iliyochanganywa mahindi, ngano, mtama, soya, Karanga, na Mchele. Je kwani vina madhara kwa mtoto. Naomba Msaada tafadhali.

  205. Pole na majukumu. Mtoto wangu alizaliwa na tundu dogo kwenye moyo najitahidi sana kumlisha lakini hanenepi. Shida inaweza kuwa ni nini?

  206. Asante kwa masomo yenu mazuri. Naomba kujua kwa nini mtoto wangu kavimba fizi kama jino linaota? Anazo siku kumi na nne tu.

  207. Hello, huyo mpeleke kwa daktari wa watoto maana ni mdogo sana kuwa na ukosefu wa vitamin c ambayo ndio hufanya watoto kuvimba fizi

  208. habali asante kwa somo zuri ninamtoto anamiezi nane sasa nimejalibu kumchanganyi vyakula na anakula mala tano kwa siku nimiezi mitatu mfululizo anakilo 7.5 na haongezeki japo akiwa na miezi saba aliugua sana na nilivyo mpeleka clinik bado anakilo 7.5 sijui nifanyeje ni uji upi bola kwake na nifanyeje aongeze kilo na anatatizo la kuhalisha sijui anashida gani

  209. Mtoto wangu ana miaka miwili na nusu hataku kula kabisa nimpe nini ili ale? Asateni kwa majibu mazuri

  210. Nashukuru kwa ufafanuzi nilikua naumiza sana kichwa juu ya mwanangu ale nini sasa nimeipata ratiba na nakuahidi nitaifuata neno langu la heri kwako ni ‘MUNGU AKUBARIKI’

  211. NINA MTOTO MWENYE UMRI WA MIEZI 8 NA MAMA YAKE TAYARI AMESHA BEBA MIMBA NYINGINE NIFANYE NINI ILI KUMSAIDIA MTOTO WANGU APATE KUKUWA VIZURI KWENI TAYARI AMESHA ACHISHWA KUNYONYA NAOMBA USHAURI WAKO ASANTE.

  212. Mimi ninamtoto wa miezi 8 wa kiume mpaka sasa hajakaza kukaa anaonyesha kuwa mvivu nifanyeje jamani

  213. Dada shikamoo,asante kwa somo zuri la lishe ya mtoto. Mimi ni mama mtarajiwa lakini pia ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza. Ninaomba unisaidie maana nategemea kujifungua mwezi wa sita mwishoni na baada ya hapo nina wiki kama tatu tu za kukaa na mwanangu na baada ya hapo nitakua mafunzoni kwa njia ya vitendo katika mbuga mojawapo ya wanyama ivyo mtoto atabaki na bibi yake pamoja na baba yake. je nijiandae kwaajili ya kumpa lishe gani ambayo itasaidia katika ukuaji mzuri maana sijui nifanye nini. NAomba unisaidie dada yangu

  214. naweza kuchanganya uji na maziwa ya ng’ombe au namnywesha kama ulivyo.

  215. nawapongeza sn kwa maswali mazuri ya ufahamu na majibu mzuri ya hali ya juu nimejifunza mengi sn coz mtoto wangu ndo ana miezi 3 Mungu awabariki sana ktk mambo yenu yote hususan malezi kuwa na watoto ni raha sana!

  216. Mama glen

    Nashukuru dada kwa ushauri wako mzuri kwa watoto, mimim mwanangu ana miezi 6 na nusu sasa, nimeshamuanzishia lishe ya uji wa ulizi na anaupenda kwani namchanganyia na mahindi,karanga,na soya kidogo na maziwa ukishaiva. sasa ameacha kunyonya hataki kabisa kunyonya tangu ana miezi 6 kasoro je nifanyeje ili aendelee kunyonya mwanangu

  217. mama glen Says:
    Your comment is awaiting moderation.
    July 2, 2015 at 10:08 am
    Mama glen

    Nashukuru dada kwa ushauri wako mzuri kwa watoto, mimim mwanangu ana miezi 6 na nusu sasa, nimeshamuanzishia lishe ya uji wa ulizi na anaupenda kwani namchanganyia na mahindi,karanga,na soya kidogo na maziwa ukishaiva. sasa ameacha kunyonya hataki kabisa kunyonya tangu ana miezi 6 kasoro je nifanyeje ili aendelee kunyonya mwanangu

  218. habari mama asante kwa slim nzuri, nnamtoto wangu miez 7 anatakwa na vipele shingoni na mashavun lakn nmempa uji was nafaka mchanganyiko naomba ushauri wako.

  219. Anaweza kuwa na allergy ya maziwa au karanga. Kwa ushauri wa kitaalamu muone daktari wa watoto atakusaidia

  220. Samahani kwa kuchelewa kukujibu tatizo lako naomba ukamwone daktari wa watoto kwa ushauri zaidi

  221. Thank you soon much,nice somo,nimezid kujifunza maana I have a baby with 9 month,thank you a lot.

  222. Thank you soon much,nice somo,nimezid kujifunza maana I
    have a baby with 9 month,thank you a lot.Mama Johson

  223. very detailed, am 1st time mom my daughter turns six months end of this week so i have already known how to take her through with this article. good work and god bless you

  224. habari! nina mtoto ana miezi minne sasa, ila anasumbuliwa na mafua ya kubana kiasi kwamba anakuwa anapata shida kupumua, vipi nimpatie dawa gani ili aweze kuwa vzuri, pia kuna mtu alinishauri kuwa mafuta ya samaki ni mazuri kwa watoto kupatiwa kadri wanapokuwa km kinga ya magonjwa mbali mbali, vipi kwa ushauri wako kuna umuhimu wa kumpatia mtoto mafuta hayo

  225. Hongera kwa kupata mtoto. Nakushauri kumuona daktari wa watoto kwa uchunguzi wa kina kwanini anakuwa na mafua hayo na hata siku moja usimpe mtoto dawa bila kuandikiwa na daktari. Ni hatari sana. Mueleze daktari hofu zako zote na maswali yako yote akuelekeze na kukusaidia

  226. Shalom dada
    mimi mwanangu anamiezi nane na nusu sasa uji wa lishe na mtori anakula vizuri je viazi vitam navyo nikichemsha na baadae nikisaga vikawa km mtori na nikichanganaya na supu ya nyama au samaki ni nzuri kwa afya ya mtoto?

  227. Viazi vitamu ni vizuri sana kwa afya ila kwa miezi nane usisage kwenye blender vipondeponde tu na mwiko ili azoee kutafuna asijekusumbua baadaye

  228. Mm na mtoto wa miezi mitano ningee penda kujua mtoto wangu amatakiwa kula chakula cha ainagani

  229. mbarkiwe sana, nna mtoto wa miez name ukuaji wake naona mzur tatzo mpka xaiv ajaota meno kuna madhara??

  230. Napenda sana mnavyo tu elimisha kina mama maana kina mama wengi hatujui muda wakulisha watoto kwasasa najuwa ratibu na muda wakumlisha mtoto wangu asanten sana

  231. Salon samahan ninamtoto anamiez sits lakin bado shijaaz kup chakul!je niaz nachakul gn

  232. shalom mimi nina mdogo wangu mtoto ana miezi mitatu na hashibi maziwa na ameamua kumwanzishia uji wa dona naomba ushauri jamani lishe anayoweza kumpa maana ni mfanyakazi itabidi akimaliza matenity anze kazi

  233. Asante sana mtumishi kwa kutuelimisha .nina mtoto wa miezi 6 na wiki 2. ameanza kulalia tumbo kama ishara ya kutaka kutambaa.nilimwanzishia uji wa dona akiwa na miezi minne na wiki.kwa sasa nampa pia mtori na viazi.baada ya kuanza kumpa hivi vyakula vingine, uji hautaki tena. je nifanyeje?

  234. naomba ushauri mtoto wangu hua anapungua uzito kila nikimpeleka clinic nifanyeje?

  235. Ubarikiwe sana mummy. Nashkuru kwa mafunzo yako natumai yatanisaidia.
    Niko na mtoto wa mwaka sasa kijana ile kilo yake ni 9.8kg. Utanipa ushauri yani kwa mwanangu?

  236. Ubarikiwe sana mummy kwa mafunzo unayopeana. Mungu azidi kukutumia vyema kwa kipawa hiki.

    Mwanangu ako na mwaka sasa ila weight yake 9.8kg. He has not been feeding well. Tafadhali naomba ushauri. Asante

  237. Wapendwa naomba kuelezwa hivi mtu mwenye pumu anaweza kumuambukiza mwengine maana Nina mdada wa kazi anayo nataka kujuwa zaidi kiafya juu ya mwanangu mwenye miezi saba sasa

  238. Pumu ni ugonjwa wa kuzaliwa nao na hauambukizi bali mafua ya kawaida hauambukiza

  239. shaloom
    Naitwa Glory
    mimi ni mama wa mtoto ana miezi 5 anaenda sita, Nilishauriwa na mama nikaanza kuumpa mtoto wangu uji akiwa na miezi 4, kwa sasa ana kaa na anakilo 7
    Nasikitika na nimebaki njia panda kwa kumuanzisha uji mapema,Naomba unishauri niache au niendelee. nilimuanzishia pia kumpa mtori na viazi na visaga kama uji.
    Je ni athari gani watoto wanazipata kwa kuanza kunywa uji mapema.

  240. Mama Sarah wa Kahama
    Nimependa sana mada yako ninajitahidi kufanya hivyo nitaongeza zaidi

  241. mtoto wangu ana miezi sita sasa na mimi ni mfanya kazi. maziwa yangu yamekauka kabisa hayatoki tangu nlipoanza kumuacha na kurudi kazini, nimekua nikipata shida namna ya kumbadilishia chakula nimekua nikimpa ndizi zillizopondwa na maziwa tu pamoja na maziwa na matunda kidogo but I wasn’t sure namna ya kubalance mlo wake. thanks.

  242. habari dada mi nashukuru sana kwa kutuelimisha akina mama nimepata mambo mengi sana kutoka kwako na nitayafanyia kazi mimi ninamtoto wa kike (Gladness)wa miezi minne na wiki tatu anauzito wa kilo 7.6 je nisawa na umri wake? pia yaani ukianza kula anatamani hata akunyang’anye chakula anakunywa uji wa uwele uliochanganywa na mafuta ya tan bond, pia anakunywa maziwa ya SMA maana ninafanya kazi na ninachelewa kutoka kazini hivyo maziwa yangu ameanza kuyakataa pale ninaporudi ananyonya kwakumlazimisha ila usiku ananyonya sana je? nisawa na ikifika miezi 5 naweza kumpa juice ya embe,na parachichi? japo kidogo? maana nimlaji sana naomba ushauri my dia.

  243. Wow ni elimu nzuri sana mzazi anaipata
    Hasa kwa wale ambao ni uzazi wa kwanza
    Ina msaada sana mbarikiwe.

  244. mtumishi pole sana kwa majukumu na ubarikiwe na blog yako yenye mafunzo mazuri…..mwanangu ndio anaanza mwezi wa sita ila nilimuanzishia uji wa dona kwa kuuchuja alipokuwa na miez minne maana alikuwa anasumbua sana, je kwa sasa naweza kumuanzishia uji wa ulezi kidogo+karanga na pia mtori kidogo na ratiba yake ya kula inatakiwa iweje….Ahsante

  245. Shukrani sana mtoa mada, nnimependa somo mtoto wangu anafikisha umri wa miezi sita tarehen13/06/2016. Asante na kama kutakuwa na somo jipya please tuige mifano ya wazungu kuweka vitu kwenye mtandao

  246. habari kwakweli tunafaidika sana mimi ninamtoto wa miezi saba kasoro nilimzaa njiti ila hataki kula kabisa na uzito wake ni mdg 6.69kg sijui nifanyeje na najitahidi kumbadilishia vyakula ila hataki yeyye ananyonya kidole tafadha naomba nifahamishe nn chakufanya my number 0717-903100

  247. Ahsante sana mshauri wetu, mimi nina mtoto ana mienzi nane sasa, na nilimzaa njiti na ana kilo 8, je hizo kilo ni halali kwa mtot wa mienzi 8? au ni huo uzito ni mdogo

  248. Thanks sana wapendwa mm mwanangu amefikisha miez saba na huwa nafanya hvyohivyo mm ni muuguzi nilipataga training kabla hata sijabeba mimba kwa hyoo ninashukuru hata wenzangu kama mnafanya hvyo

  249. Asante kwa ushauri wenu nafurahia sana elimu yenu na ushauri wenu kuhusu lishe je mtoto ambaye hataki kula hata alibadilishwa chakula anataka kunyonya mnashaurije?

  250. habari dada, asante sana kwa mafundisho yako nina watoto wawili wa miaka 3 na mwingine miez tisa nimejifunza mengi sana.Nina swali moja ni mchanganyiko upi wa nafaka zinawez kuwafaa wote kwa ajii ya uji. Ubarikiwe

  251. Ndugu Me Nashukuru Kw Ushaur Bora. Lakin Swali Langu Nataka Kujua Je Kuna Madhara Gani Kw Mtoto Anayenyonya Kama Wazazi Watakuwa Wanafanya Tendo La Ndoa?

  252. nimependa sana ufafanuzi na maelezo haya muhimu sana….

    sijatoka bure…

    Nimejifunza mengi sana.

  253. jamani mtoto wangu haongezeki uzito.nampikia chakula ila anakula kwa shida sana.nisaidie ni vitu gani naweza mpatia uzito ukabadilika.mtoto anazidi kuwa mdogo badala ya kukua

  254. Nashukuru sana kwa ushauri mzuri kuhusu lishe za watoto. Nimejifunza kitu hapa. keep it up.

  255. Asante kwa ushauri nzuriii xn mtoto wng anamiezi sita na ana kilo 9.9 na hajaanza kula hii inamadhara docta maana nataka nianze kumpa ujiii mda wa kula tayarii

  256. Mtoto wangu anapungua kilo haendi saw a na Graff na anapata mlo vizuri japo muda mwingine anachagua chakula ..ana miezi 10 nisaidieni tafadhali

  257. Ubarikiwe saana. Nimejifunza mengi sana mie mwanangu ana miezi mitano wiki mbili anatumia maziwa yangu. Naweza kuanzisha supu kwa sasa?

  258. NASHUKURU SNA.TUNAOMBA MUENDELEE KUTUELIMISHA ZAIDI JUU YA MAKUZI YA WATOTO WETU PIA.

  259. naitwa Idd hashimu nauliza kuhusu mtoto mwenye umri wa mwaka nanusu kila nikimpeleka kupima uzito unaongezeka nusu asaivi anauzito wa kilo saba na nusu je nitatizo gani kwasababu mwaka na nusu anatakiwa awe na kilo kumi na kuendelea

  260. Asante Sana kwa ushaur wenu ila nina swali,
    ‘Mama anayenyonyesha anaumwa na ana2mia dawa sasa mtoto anapo nyonya yale maziwa hayawezi kumletea madhara ?

  261. ninaomba msaada nimekutana na situation especial kwa watu wenyekipato cha chini sana kwamba anajifungua mtoto halafu maziwa hayatoki kabisa na anakuwa hana uwezo wa kununua maziwa ya formula kwasababu anauwezo mdogo sana. hili tatizo ni kubwa sana na maranyingi kwa mazingira niliyoko linasababisha watoto kuugua. naomba ushauri wa kitaalamu watoto kama hasa wanapewa chakula gani, maana tumeelimishwa kuwa maziwa ya ngombe si masure kwa mtoto mdogo sana. naombeni msaada wa kitaalamu

Leave a comment